constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
18

Ma-DC na Ma-PC wapitie Bunge. Wale ambao wanataka hiyo kazi, waombe katika Bunge, ijadilie jambo hilo ili kupatikane

mtu ambaye ana kiwango ambacho kinawezekana na hiyo kazi. Kwa hivyo hayo madaraka yasiwe ya Rais, iwe katika Bunge.

Katika mashamba, kila mtu awe na uhuru wa kununua shamba popote pale katika nchi ya Kenya, mahali ambapo anafaa akae.

Thank you.

Com. Bishop Njoroge: Thank you very much Paul. Jacob Partimo karibu.

Jacob Partimo: Kwa majina mimi naitwa Jacob Partimo Munge, mkaaji wa Loitoktok. Ningependa kuchangia nikisema ya

kwamba, kile ambacho ningependelea Katiba ichukue ni kuwe na Serikali ya Majimbo. Ninaposema Majimbo, nasema

kwanzia ngazi ya Mkoa, hadi katika kijiji. Rasilimali zilizoko, ziweze kutawaliwa na lile jimbo, iweze kusaidia wakaaji wa ile

sehemu. Mauzo za rasilimali hizo, ziuzwe katika vijiji. Wazee wa vijiji wanajua vile watakavyoweza kusaidia kila familia iliyoko

pale.

Ningelipendelea pia katika Katiba ya kwamba, masomo yawe ni ya bure, kwanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu na kuwe -

tuangalie kuna sehemu zilizoendelea tangu wakati wa ukoloni. Unakuta mtoto wa Kajiado ambaye amepata B + hapati nafasi ya

kuingia katika chuo kikuu. Kuingia katika Chuo Kikuu iangaliwe kulingana na kadiri na vile watu walivyo. Pia ningeweza

kusema ya kwamba, Serikali iliyoko katika mamlaka, itupilie kitu kinachoitwa soko huru. Iweze kutunza wananchi wake.

Wanyama pori: wanaua binadamu na malipo ni shilingi elfu thelathini. Napendekeza hizo sheria zinatudhulumu hivyo, zitupiliwe

na iwe ni zaidi ya shilingi milioni tano kwa binadamu mmoja. Pia mifugo na uharibifu wa mashamba uweze kutunzwa. Wawe

compensated. Serikali pia iweze kulinda haki ya kila mmoja. Ninaposema hivyo, nasema ya kwamba sheria za Ma-Chief, ziwe

kama zilivyokuwa hapo awali. Sio ile ya 1998. Ili kuweza kutunza kila mmoja. 75% ya sheria za nchi hii ambayo inahusu

Commissioner wa Ardhi ama Waziri wa Ardhi, aweza kutangaza sehemu kuwa ni sehemu ya wanyama wa pori. Hiyo sector

itupiliwe kwa sababu wanakijiji wanajua manufaa ya hiyo ardhi.

Kazi: Kazi, kulingana majimbo - mahali ambao umetoka, upate kazi pale lakini wataalamu wawekwe katika Serikali kuu.

Asilimia sabini na tano, ipewe wenyeji. Rasilimali zilizoko katika sehemu, wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuziuza. Kwa

mfano mali wauze na wafanye matumizi katika kujiendeleza hali yao.

Habari ya uuzaji wa ardhi: Nilisema ya kwama wanakijiji waweze kutawalana ndio tumesema Serikali ya Majimbo itoke

kwanzia vijijini mpaka mkoani. Asante.

Com. Bishop Njoroge: Umesema kwamba rasilimali ziwe za jimbo na jimbo litawale hizo rasilimali. Unaweza kutuambia,

kama tutakuwa na Central Government, na Central Government itakuwa ni nini? Pia ningetaka kukuuliza, kama yale maji

inakunyiwa Nairobi, inatoka Mt. Kenya na watu wa Central Province wakipewa ruhusa ya kutawala hayo maji, inaweza