constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
27

Kuhusu masomo: Masomo kulingana na vile ninaona ya kwamba, masomo katika Kenya tunaambiwa ni ya bure lakini tunaona

bado haijakuwa ya bure. Masomo tungependa iwe ya bure kwa sababu watu wengi katika Kenya hawana rasilimali, hawana

mapato. Na tunaona watoto wao, hasa ndio unakuta wanapita katika shule. Lakini kwa sababu ya kuwa hawana mapato,

watoto hao wataendelea na masomo. Kwa hivyo masomo iwe ya bure.Vile vile, matibabu. Tunaona ugonjwa hauchagui tajiri

kwa sababu ndio ana pesa ya kujitibu. Tajiri na maskini wanapatwa na ugonjwa hali sawa. Kwa hivyo ningependekeza

matibabu yawe ya bure. Ili watu waweze kuokolewa maisha yao.

Kuhusu ardhi, kusema ukweli ardhi ya Wamaasai, imenyakuliwa kwa njia ambayo hatujui imetokana na nini. Kwa sababu

wanyama sio eti kwamba wanyama wanazaliwa Maasaini peke yake. Lakini tunaona ya kwamba ardhi yetu iliyonyakuliwa kam

Amboseli na Tsavo West National Park, tunaona ni ardhi ambayo ingeweza kusaidia wananchi hasa katika hali ya kilimo na

kupanda miti rasilimali ya aina mingi, tunaona ardhi yetu imenyakuliwa ambayo tunaweza pata manufaa nayo. Ningependekeza

hiyo ardhi irudishwe kwa wenyewe. Maana tangu Wamasai walipopatikana, hakuna siku Maasai amekuwa adui na mnyama na

ndio maana kwao ndio wanyama wanabaki. Na watajua vile wataendelea kukaa na wanyama.

Kuhusu MPs, ningependekeza kuwa, uchaguzi unapofanyika, Mbunge achunguzwe na watu wake kwa miaka miwili,

akionekana hakuna kazi anaweza fanya, itolewe kura ya kusipokuwa na imani naye, aondolewe. Ili wananchi wasiendelee

kuumia kwa muda huo wote. Kwa sababu kama wananchi watakuwa wakikaa kwa miaka mitano katika taabu, hata mwezi

mmoja ni shida licha ya miaka mitano. Unakuta…..

Com. Bishop Njoroge: Nakupatia dakika moja.

Isaiah Ole Samana: Hata hivyo nimemaliza. Kwa hivyo ningependekeza ya kwamba iendelee. Kuhusu mambo ya Ma-Chiefs,

Ma-Chiefs waendelee kwa sababu wao ndio wanaelewa shida na taabu ya familia zile ziko karibu na wao. Wao ndio wazaliwa

na wanajua shida, na umaskini na unyanyasaji wa wale watu. Kwa hivyo ningependekeza Chief aendelee kubaki, Provincial

Administration yote kutoka Sub-Chiefs, mpaka Province iendelee. Asante.

Com. Lethome: Ngojea kidogo kuna swali hapa. Kuhusu zile National Parks, wasema ardhi ya Wamaasai, warudishiwe

Amboseli na Tsavo. Wa-Sumburu nao wakisema yao warudishiwe, Meru National park warudishiwe. Unapendekeza yaani

Kenya tusiwe na any National park ama vipi? Kwa sababu it has to be curved out kutoka kwenye ardhi ya watu fulani. Kwa

hivyo unapendekeza katika Kenya tusiwe na National Parks zozote ama vipi?

Com. Bishop Njoroge: Ningetaka kuongeza hapo, katika mapato mengi kutoka National Park, zinaenda kwa Central

Government na ndio expenditure ya Serikali inatokana hapo. Hivi ni kusema kwamba mapato hayo sasa haitakuwa ya

CentalGovernment, ungetaka iwe ya Jimbo, kwa hivyo Central Government itafute njia kufanya mapato yake.