Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
54

milango ya milele; na mfalme wa utukufu ataingia. Nani aliye mfalme wa utukufu?

Bwana mwenye nguvu na uwezo, Bwana mwenye uwezo vitani. Nyanyulisheni vichwa

vyenu, ee ninyi malango, ndiyo, muvinyanyue, ninyi milango ya milele, na mfalme wa

utukufu ataingia. Ni nani huyu mfalme wa utukufu? Bwana ya majeshi, yeye ni Mfalme

wa utukufu. Sela.

ZABURI 116, 10-19

Ninaamini, kwa maana nitasema: Niliteswa sana: Nikasema katika haraka yangu:

Watu wote ni wawongo. Nitamupa Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?

Nitapokea kikombe cha wokovu, na kuitia jina la Bwana. Nitalipa Bwana naziri zangu,

ndiyo, mbele ya watu wake wote. Ni ya damani machoni mwa Bwana mauti ya

watakatifu wake. Ee Bwana, kweli mimi ni mtumishi wako: Mimi ni mtumishi wako,

mwana wa kijakazi chako; umefungua vifungo vyangu. Nitakutolea zabihu ya kushukuru,

na kuita jina la Bwana. Nitalipa naziri zangu kwa Bwana, ndiyo, mbele ya watu wake

wote; katika viwanja vya nyumba ya Bwana, katikati yako, ee Yerusalema. Musifu

Bwana.

Utukufu. . . Sasa.. . Alliluya (mara tatu). Utukufu kwako, ee Mungu. Bwana

hurumia (mara tatu)

Kiisha anza kuimba nyimbo zifuatavyo: Sauti ya sita

Zarau wovu wangu, ee Mungu wewe uliyezaliwa kwa Bikira, takasa roho yangu,

ulifanye hekalu ya mwili na damu yako kuwa takatifu, kwa hasira yako usinitupe mbali

ya uso wako, wewe mwenyi huruma usiyokadirikana kisilani mbele ya uso wako, wewe

uliyekuwa na huruma yasiyo kipimo.

Utukufu kwa Baba na kwa Mwana na kwa Roho Mtakatifu.

Nitasubutu je, mimi mwovu, kujongea mafumbo yako Takatifu? Nikijaribu

kujongea pamoja na wenye kustahili nguo yangu itanitoa maana haiko ya arusi. Na

nitavuta mbegu ya hukumu kwa moyoni mwangu mtenda zambi nyingi. Ee Bwana,

takasa roho yangu yenyi kuchafuka na uniponye kwani wewe ni mwema na Mpenda

wanadamu.

Sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina. THEOTOKION

Ee Mama wa Mungu, zambi zangu zinapita wingiu; ninakimbilia kwako Mtakatifu

kwa kutafuta wokovu. Angalia moyo wangu wenye kushikwa na ugonjwa na uniombee

kwa mwana wako, Mungu wetu, anisamehe mabaya yote niliofanya kwako, ewe

Mbarikiwa.

Paka siku kubwa ya kazi Ine Takatifu wanaongeza kusoma: Sauti ya Mnane.

Mitume watukufu waliangazwa, wakati walioshwa miguu ku karamu ya mwisho,

kwa ile wakati Yudasi kafiri, kwa tamaa yake mbaya, akaingia gizani na akakutoa

wewe mwamuzi wa kweli, kwa mwamuzi waovu. Ee mnyanganyi, tazama ni kwa sababu

ya hii amejitundika: Epuka tamaa iliyomuongoza kutendee Rabo wake maovu ya hii

namna. Ee Bwana mwema wa wote, utukufu kwako.

Bwana hurumia (Mara 40)