Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
5

vile?” “Kwa nini tunaamini dhambi ya asili?” na “Kwa nini wanadamu

wamelazimishwa wakubali ‘dhambi’ za Adamu na kisha matokeo yake

waadhibiwe milele?” Lakini kama utamuuliza mtu yeyote maswali hayo,

watakujibu kuwa unalazimika uamini bila ya kuhoji, au kuwa hiyo ni “siri

isiyoelezwa” na hutakiwi kuuliza “Kaka wewe amini tu.”

Maana ya Utatu

Jambo la kushangaza sana, neno ‘utatu’ halimo katika Biblia. Na limekuwa

likihusishwa na wanazuoni wa kidini mapema mnamo miaka mia mbili baada

ya kunyanyuliwa kwa Yesu kwenda kwa Mungu wake Muweza.

Ningewaomba wahubiri na wachungaji wanipe japo fikra, vipi ‘moja’

itapigwa hesabu ili iwe ‘tatu’ au vipi Mungu mwenyewe awezaye kufanya

kila kitu atakacho, hawezi kuwasamehe watu na dhambi zao, isipokuwa hadi

ajifanye mwanadamu, aje chini duniani, awe mtu, na kisha achukuwe

madhambi ya watu wote; huku tukiweka akilini kuwa pamoja na hayo yote

yeye ni Mungu wa Ulimwengu wote na anafanya atakalo kulifanya, popote

pale, ndani na nje ya ulimwengu kama tunavyojua. Hao wahubiri na

wachungaji kamwe hawaonyeshi kuwa wataweza kuleta kitu kingine zaidi ya

maoni yao au mlinganisho wa kiajabu ajabu.

Baba - Mchungaji Msimikwa Asiye Na Madhehebu

Baba yangu alikuwa mchangamfu sana katika kuunga mkono kazi za kanisa,

na hasa hasa vipindi vya shule ya kanisa. Akasimikwa ukasisi katika miaka ya

sabini. Yeye na mkewe (mama yangu wa kambo) walikuwa wanawajua

wainjilisti na wahubiri wa kwenye tv wengi, vilevile wameshamtembelea Oral

Roberts na wamesaidia kujenga ‘mnara wa sala’ katika Tulsa, pia walikuwa ni

waungaji mkono imara wa Jimmy Swaggart, Jim na Tommy Fae Bakker,

Jerry Fallwell, John Haggi na Pat Robertson.

Kukutana na Mtu Kutokea Misri

Ilikuwa ni mwanzoni mwa 1991 pale baba yangu alipoanza kufanyabiashara

na mtu kutoka Misri na kuniambia kuwa anataka nikutane na mtu huyo. Wazo

hilo lilinivutia kwani niliwaza juu ya wazo la kuwa na ladha ya kimataifa.

Unajua tena, mapiramidi, Sphinx, mto Naili na mengineyo.

Alikuwa ni ‘Mwislamu’: Watekajinyara, Walipuaji mabomu, Magaidi,

na ni nani ajuaye kingine ni nini?