13.07.2015 Views

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

106Katika hizi uongozi iwe vile vile. Tunaomba nafasi ya Bunge, walemavu watengewe nafasi zao asilimia kumi na tano. Iwe nispecial ya walemavu. Katika council, asilimia kumi iwe ya walemavu kwa sababu tukisema kuwa eti pengine tungojeenomination, kulingana na iendavyo, huenda ikaja mpaka hii nominated ikawa imekatwa. Utakuta mlemavu amewekwa nje. Nakama amewekwa nje itakuwa yeye hakuna lolote analofanya kwenye serikali. Katika mikutano yote ambayo inapangwa yakiserikali, mlemavu ahusishwe pale kwa sababu utakuta mikutano mingi lakini ikiwa sheria iko, kila division, kila chiefatahusisha walemavu walio kwenye location zake ama division yake.Pia ningeomba katika mijadala mingi ambayo inaendelea, upande wa akina mama ijapokuwa hutajwa akina mama tukaambiwapia sisi walemavu tuTumehuku upande wa akina mama. Lakini ujue pia walemavu wako pia akina baba. Tungeomba hao naopia waweze kutengewa fursa zao kwa upande wa kipato kwa sababu kama hana kazi na hana shillingi yeye atategemea nini?Kupangwe angalau allowances fulani za walemavu waweze kujitegemea badala ya kutegemea omba omba.Ningeomba pia humu majumbani. Narudi chini upande wa elimu kuwe na sheria sasa ambayo itawafanya wazazi walazimishwekupeleka watoto wao walemavu shule kwa sababu hiyo iko kwa watoto wote lakini haikusisitizwa kwa walemavu kwa sababukama hivi sasa mtu akipeleka mtoto wake wa kawaida kama hakumpeleka shule utakuta yuashughulikiwa alazimishwaampeleke lakini mtoto mlemavu hashughulikiwi kabisa. Kwa hivyo naomba hiyo fursa ipatikane ya mtoto mlemavu kutoka kwama-chief wenyewe wazee wa vijiji wawe watachukua hiyo nafasi mtoto wa mlemavu apate kwenda shule. Asanteni.Com. Baraza: Asante bwana Juma. Nimeelewa maneno yako na tutayapeleka kule. Taithi Mwachimonje.Mr. Mwachimonje: Mimi nimefika hapa kwa maneno kidogo tu lakini ambayo ni mengi. Jambo la kwanza ninasema kuwatunataka ile serikali inayoitwa Majimbo. Kwa hivyo kwa kuwa watu wengi wameeleza, mimi ni kutaja tu hilo jina na mengineyameendelezwa mbele. Kitu ambacho kimenileta hapa nimeomba hii Commission iweke sheria ambayo itatunga Commissionwakati ujao, PC awe anachaguliwa na Commission badala ya kuandikwa ni Rais. DC awe anaajiriwa na Commission na DOawe anaajiriwa na mission.Jambo lingine nimekuja hapa kusema hivi, wakati ujao, hii Commission iweke sheria hivi, msitu ya forest. Forest tangu zamaniilikuwa misitu yetu na ikachukuliwa na serikali eti italindwa lakini kufikia sasa, misitu hiyo forest sasa zime-jam inachezewa nandovu. Sasa kile kitu tunataka Katiba ijayo itunge Katiba kuchukua hii misitu ya forest irudishwe kwa wenyewe wa kawaidamisitu yao. Kwa sababu ikiendelea kukaa hivyo kutakuja kuwa na uwezo wa serikali kugawa misitu ile kwa watu wengine.Kwa hivyo tunataka hiyo msitu turudishiwe wenyewe.Namba nyingine inasema hivi, hawa ndovu ni wanyama wa serikali. Ndovu hawa wametutia umaskini mwingi sana na wasiwasimwingi hata kama wengine tuko hapa, tuna woga wa kwenda nyumbani jioni sana, unaweza kukutana naye. Kitu ambachonimekuja kuomba Commission hii, ipitishe sheria katika ndovu hawa watengwe sehemu zile zenye na watu wapelekwa katika

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!