13.07.2015 Views

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

123Kwa sababu nikisema hivyo, hapa hapa tulipo, tunaishi na tunaishi na wanyama kama ndovu, na vile tunavyojua hapa kwetuakiua mwanadamu watakuja watu wa wizara ya wanyama watatu wanne na landrover yao moja. Lakini ndovu wakifa, hata DChakai hapa. mtu akiuawa na ndovu alipwe pesa za kutosha, sio shillingi elfu thelathini kama ambaye ni mtu amekatwa kidole.Com. Swazuri: Alipwe pesa ngapi?Mr. Baguani: Milioni tatu. Na ikiwa ndovu hao hao wameharibu mashamba ya watu moja kwa moja ripoti hii ikipelekwa,utaratibu uchukuliwe na mwenye aliyeharibiwa mimea yake alipwe kwa sababu watu huwa wanapata taabu, ametegemeashamba na limechafuliwa na ndovu, hana chakula, hajui atapata wapi uniform ya watoto wala si ya watoto, sasa yeye ni mtuanakuwa anadhulumika. Ingine, Majimbo yakija na ikiwa mamlaka ni ya kimajimbo urongo, mambo mengine yatafanyikakirahisi maanake hapa kwetu Pwanimkoa ni mkubwa kutoka kizingitini mpaka lamu, kutoa mombasa mpaka taita. Ni njiachache sana ambazo zinapitika. Barabara hakuna na ukweli ni kwamba hata sasa kuna hospitali nyingine mtu akipata faradhiamekufa, inabidi mtu yule achukuliwe na baiskeli apelekwe mahali atakapokwenda zikwa.Ni jambo la kusikitisha sana kuona tangu uhuru mpaka sasa kuna sehemu nyingi hazifikiki. Ingine tena katika mkoa kwa mfanomkoa wetu wa Pwanitunashangazwa na kitu kimoja sisi, maji mengi yanayotoka sehemu za mlima, maji mengi yanayotoka hapahapa kwale yanapitishwa chini kwa chini mpaka Mombasa na katikati hii kuna wadigo na waduruma pamoja na ndugu zao wakikamba ambao ni wa hapa hapa Pwaniwanakosa maji. Ni jambo la kusikitisha, lakini ikiwa umekuwa ni utawala wa kimajimbourongo sehemu nyingine zitatengenezeka, hata ijapo inchi yetu imekuwa dhaifu, imekuwa na ufisadi mwingi lakini sidhani kamamtu anaweza kukoka moto na akajichoma mwenyewe. Mengine nitasema wakati mwingine asanteni.Com. Swazuri: Asante sana. Sasa tuna Hassan Haji Masa.Mr. Hassan: Asante sana makamishina wote wawili na wageni waliofika. Mimi sina maneno mengi sana mengiyamezungumzwa. Jina langu naitwa Hassan Haji Masa. Kwa sababu mengi yamezungumzwa, mimi nitazungumza kama matatuhivi. Na ni kuongezea tu lakini yameshazungumzwa. Kwanza ni upande wa utawala. Mfumo wa serikali. Serikali ninayohitajimimi katika mawazo yangu ni Majimbo. Majimbo maana ndicho kitu ambacho kitakuwa kitamfanya kila mwananchi ili awezekufaidi katika haya matunda ya uhuru.Kwa upande wa Majimbo, tumezungumza kwamba ma-governor wawe kama vile walivyotajwa kwamba kila jimbo liwe nagovernor, ikiwa Majimbo ni yale manane basi governors wawe wanane basi governors wawe wanane lakini kwa upande waRais ambaye atakuwa katika central government, mimi katika maoni yangu kwa sababu sisi sote ni wananchi wa kenya,Majimbo yote manane ni ya watu wa kenya ili kusiwe na wasiwasi na ikiwa tunapendana kwa kweli kabisa tuwe katika kilecheo cha uRais, kiwe kinaweza kuzunguka kwa Majimbo yote.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!