13.07.2015 Views

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

68Kwanza langu mimi nitazungumzia kuhusu mambo ya ardhi. Ardhi katika huu mkoa wa pwani. Kutoka zamani ilipoanzakutawaliwa na mreno, akaja mwarabu, akaja mwingereza kisha tukanyakua uhuru. Ardhi hizi zilikuwa zikimilikiwa kwa njia yavile walivyojichukulia wale watawala wa kiarabu na mpaka sasa ukiangalia kutoka Vanga mpaka Lamu ardhi hizo wenyejiambao halisi ni wazaliwa wa hapa, wadigo na waduruma, ardhi hizo hawanazo hata kidogo bali wao ni watumishi katika ardhihizo.Pendekezo langu mimi ninalolitoa ni kwamba kulingana na Katiba mpya ambayo itatolewa,vile walivyozipata ardhi zile kulinganana serikali ile ya ya waarabu wakati ule, sheria irejeshe upya kwamba ardhi hizo zirudishwe serikalini na ziweze kugawiwawenyeji kikamilifu na kupata title deed zao ili kuwe na kwamba kila mmoja ana haki kuliko yule aliyetoka kutoka uarabuni amauingereza ama mahali pengine aje awe na haki kuliko mzaliwa wa hapa awe hana haki.Jambo langu la pili, ni ardhi hizi za serikali ambazo ni state land. Wakati tuliponyakua uhuru kulikuwa na mtindo kana kwambakunachukuliwa ardhi fulani za serikali zigawiwe wananchi wale ambao wanaitwa squatters lakini hawa kufikiriwa wale squattershalisi ambao walikuwa wakiishi ndani ya yale mashamba Commissioner of lands ndiye alikuwa akichukua uwezo wa kuonakwamba ardhi hizo ikiwa kuna jamaa zake ama kina nani wameomba hizo ardhi basi wawe wanapatiwa / letters wanaenda kuletayari shamba ni lake lakini yule mwananchi wa kawaida ambaye ni mzaliwa wa pale amelima pale, ana mimea ya kudumu pale,wakati ule ule yeye hastahili pale ataambiwa hapa ni pangu ondoka. Kwa hivyo jambo hilo lifutiliwe mbali, ardhi zile kwanzazipawe wale ni squatters pale ili wajisikie kwamba wana haki kama mkenya mwingine.Jambo jingine, ni mambo ya utawala. Kwangu mimi nasema ni haki kabisa wakati huu tuwe na serikali ya Majimbo lakini Raisaweko na kuwe na prime minister wagawiwe madaraka ili kuwe na kwamba kila mmoja akatekeleza kazi zake vile ambavyoatakuwa amepangiwa kulingana na sheria ya nchi yetu kwa sababu hivi sasa ukiangalia kweli kila kitu kiko kwa Rais since he isabove the law lakini ukichunguza tena hapo hapo, kibinadamu kuna wengi ambao wamepewa nafasi na vyeo kupitia kwaserikali kuu na Rais amesema okey, wewe shika hii, shika madaraka haya, wale wale wanatupanisha madaraka yao akijisikiapengine Rais ni mjomba wake ama ni kakake, sasa utaona mali nyingi zinaporwa na mtu akipelekwa mahakamani hakuna kesiitakayomshinda mtu yule kuona kwamba amepatikana na hatia aweze kupelekwa gerezani na mali ile irejeshwe kwa serikali ilikuona kwanza umma utaweza kufaidika. Kwa hivyo Rais aweko lakini asiwe above the law.Ukirudi upande wa polisi, polisi ukweli hivi sasa kuna haja ya mabadiliko makubwa kuhusu sheria zinazofuatiliwa na polisi. Sisiwenyewe Commissioners ambao mmekuja hapa mmejionea wenyewe barabarani. Polisi sasa ni kuwa kila saa kumi na mbiliawe barabara ahakikishe ikifika saa nne saa tano ameshatengeneza karibu elfu saba wanaondoka na pesa zile haziendiserikalini. Na gari lishtakiwe liliyo na makosa, lipelekwe mahakamani, pesa zile ziweze kupatikana kwa kuhudumu serikali lakiniutakuta sasa ni mtindo wa kubagua shillingi mia mia watu wakiokota na serikali bado inataabika pesa hakuna. Miminapendekeza kuwe na mahakama ya mobile.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!