13.07.2015 Views

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

91Haki za binadamu- serikali ina wajibu wa kuelimisha watoto wa kenya bila kujali rangi, kabila ama maumbile, katika shule yamalezi mpaka chuo kikuu. Serikali iangalie maslahi ya wale watu wasio na kazi ili wasiwe wezi kwa hivyo wapatiwe allowancemtu ambaye hana kazi. Kila mtoto anayezaliwa apatiwe allowance ya kumwezesha kukua. Kila mkenya awe na haki ya kupatamatibabu ya bure. Kila mkenya ana haki ya kuchangia maendeleo ya uchumi wa kenya. Asanteni sana.Com. Swazuri: Asante sana mama. Munyole Tabu na atafuatiwa na Omari Saidi.Mr. Munyole: Makamishina, mabibi na mabwana salaam aleikum. Mimi yangu ni mambo mawili tu. Kwanza ni mfumo wamaongozi. Mfumo wenyewe tunataka Majimbo. Pili, ni lugha ambayo tunataka ifundishwe katika kila jimbo. Tunapenda lughaambayo tunataka ifundishwe katika nini kila jimbo. Tunapenda lugha ya mama ifundishwe kwa maskuli, kwa sababu nchi zilezimeendelea wanazungumza lugha zao na wanafundisha lugha zao mashule. Ndio sababu, from the word go mtoto anajua,anakuwa mwerevu kwa sababu anafundishwa lugha ya mama. Kwa mfano, hapa sasa hivi kuna wazee wengi ambao hawawezikuzungumza Kiswahili ama kizungu wakifahamu hawawezi kuelezea vile ambavyo wanataka Katiba iundwe. Kwa hivyo sasautakuta watu wengine wamekaa na hawawezi kuzungumza kwa sababu ni lugha zile zinafundishwa shule ni geni. Kwa mfano,kizungu.Com. Baraza: I want to interrupt you. Kama hujui kizungu au Kiswahili uko na haki ya kusema mambo ya Katiba kwa lughayako. Usikae hapo umeogopa kwa sababu hujui kizungu ama Kiswahili hiyo itakuwa ni makosa. Nilisahau kuwaeleza, ongeakwa kidigo, ongea kwa kichonyi, tutaelewa tu.Mr. Munyole: Sasa mimi nataka kuongea kidigo. That one is very important because wengine hawakusoma kabisa. Sasatunataka hii Katiba mpya itakayotungwa ya Majimbo wawe shule wanafundishwa kidigo. Hesabu mwanafunzi awe anaelezewakidigo na masomo mengine. Hata sayansi iwe ni kidigo ndio mwanafunzi ataweza kukutana maprofesa wengi kuliko sasa. Kwahayo machache asanteni.Mr. Omari Said: Kamishina na wasikilizaji salaam aleikum. Mimi naitwa Omari Said Rua kutoka Gombeni location. Mwanzonitazungumzia serikali na sitazungumza mambo marefu kwa sababu mengi yamepitiwa na wenzetu. Kitu cha kwanza, serikalitunayohitaji sasa ni serikali ya Majimbo na ziko sababu mbili ama tatu kwa nini tunahitaji serikali ya aina ya Majimbo. Sababuya kwanza, serikali ya mfumo tulio nao imewaacha watu wa Pwaninyuma.Imetuacha nyuma kimaendeleo, kiutajiri na kadhalika. Kwa upande wa ugawanyaji power, au ugawanyaji uwezo tunaonakwamba vitu vingi vimelemea juu. Kule kwa wenzetu tunaona ya kwamba upande wa maintenance wa vitu vya kimaendeleokama barabara, utakuta hata chooni lami imefika huku lakini sisi barabara ambayo inaenda kwa DC kutoka wakati wa uhuruilitiwa juzi. Kama hii yetu hapa. Kwa hivyo tunahitaji Majimbo ili ugawanyaji uwezo upatikane nasi tuweze kula matunda ya

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!