13.07.2015 Views

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

115itilie mkazo hata katika hii Katiba yetu. Wapewe adhabu kali. Wazazi wanaoingilia watoto wao kimwili wapewe adhabu kamahiyo ya kunajisi, adhabu kali. Katiba mpya ikomeshe tabia ya kufanya mapenzi waume kwa waume yaani homosexuality, aumke kwa mke that is lesbianism au ndoa hizi za aibu. Watu hawa wakipatikana wafungwe maisha maana hawana maana humu.Kuna wanawake wengine wanaolipa mahari ili kuoa wasichana wadogo na wale wasichana wadogo kwa kuwa yeye nimwanamke amemuoa msichana mdogo, anawawacha watembee na yeyote ili wawazalie watoto. Haya huwa hasa inafanywa nawanawake ambayo hawakubahatika kupata mtoto badala ya kuenda kufanya adoption anachukua msichana mdogo halafuanamwachilia huru ili awazalie watoto.Hii ni tabia ya kinyama na adhabu kali sana ifanywe kwao. Mume yeyote asimpige na kumnyanyasa mkewe nyumbani nakumjeruhi mwili. Huyu mume amlipe gharama mkewe na pia achapwe viboko ikiwezekana ili ayasikie maumivu hata yeye yaleambayo mwanamke anayasikia kwa kupigwa. Yaani hii Katiba yetu iangalie sana, kuna wazazi ambao wanawatendea kinyamawaoto wao ama pengine mtoto wa kambo. Mtoto amechelewa lakini yeye anamwadhibu vibaya ama pengine kumpeleka shulehampeleki ama hampatii zile basic needs za sawa.Umilikaji wa ardhi- hatutaki raia wa kenya awe squatter wa mtu mweupe au mtu yeyote ambaye hatoki ama haishi sehemuinayoishi wanaoitwa masquatter. Hakuna squatter anayeishi kwenye shamba iliyoishi babu ama wazazi wake pia. Ugawaji waardhi, wahusishwe wenyewe wa pahali hapo panapogawanywa hiyo shamba na ikiwezekana wenyewe wapate ardhi ile sehemuyao. Hatutaki kunyanyaswa na ardhi yetu na watu kutoka wilaya nyingine na mikoa mingine. Na vyeti vyote vya kumilikimashamba yaani title deeds zitolewe wilayani sio Nairobi. Utakuta kuwa kuna mashamba mengine yale ya kawaida ambayoyalitumwa kawaida, title deed zinaletwa hapa. halafu kuna yale mashamba ambayo yanapimwa kwenye meza title deed zakezinapatwa Nairobi. Yaonyesha kuwa hapo kuna unyanyasaji ama kuna uporaji mali ya wenyewe.Magonjwa ya kuambukiza yasio tiba kama ukimwi. Sheria iwekwe na kuzingatiwa katika Katiba mpya kwamba yeyoteanayepatikana na hatia ya kumwambukiza mwenzake ugonjwa kwa kudhamiria iwe kwa kumnajisi ama kwa kukusudiaahukumiwe na apate adhabu kali sana ama hata ahukumiwe kifungu cha maisha hata kifo. Ukahaba au umalaya, upigwemarufuku katika Katiba hii mpya ya kenya. Utakuta hivi sasa tunawapatia majina yaani tunatoa majina kama Malaya, tunawaitacommercial sex workers ili watu waendelee ku-practice umalaya, hiyo hatutaki. Katika Katiba hii yetu mpya hiyo ikomeshwekabisa na anayepatikana akiuza mwili wake ama kufanya biashara ya kuajiri wasichana wadogo wampatie pesa kwa kufanyaumalaya ahukumiwe kifo.Tunataka iwe ni sheria, wakenya kuvaa mavazi ya heshima. Vazi linaloonyesha matusi na kuleta hamu ya ubakathi lipigwemarufuku katika Katiba yetu na tunasema kuwa kiswahili iwe ni lugha ya taifa na kiingereza iwe ni lugha ya ofisi. TunapendaKatiba mpya iandikwe kwa lugha ya kiingereza na kiswahili. Pia lugha hizi mbili ziwe rahisi na kueleweka. Hapo nyuma Katibailikuwa ni kama ambaye inasambazwa kiuchoyo ndio maana hivi sasa civic providers wamepata shida kabisa kuelimisha mamboya katiba.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!