13.07.2015 Views

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

58Com. Swazuri: Andika jina lako pale. Halima Chivumbe.Mrs. Chivumbe: Jina langu naitwa Halima Chivumbe, mimi ni kiongozi wa akina mama wilayani Kwale. Maoni yanguningependa serikali hii ambayo tuko nayo katika Katiba hii ibadilike na iwe serikali ya Majimbo. Tukisema Majimbo hatujasemawatu wa bara waende kwao lakini bado tunasema kwamba hapa si kwao. Kwa hivyo tunasema 75% ya chochote katika jimbohili la Pwanilipatiwe wenyewe wa Pwanina labda 25% tupatie wageni wetu kwa sababu si vizuri hata kule manyumbani mwetuhuwezi (spoke in kidigo)Halafu katika hiyo hali ya serikali ya Majimbo, tukasema kwamba katika mali zetu hizi ambazo ni za asili kama vile kilindini nasehemu zinginezo watu wenyewe wa jimbo la Pwani au katika serikali ya Majimbo tupatiwe mamlaka zaidi ya kumiliki vituvyote katika jimbo hili. Tunakuja sasa upande wa utalii. Utalii ni sector muhimu katika hii sehemu yetu lakini utaona mwenyehapa hanufaiki na chochote kwa hivyo mimi bado nasema kwamba katika hali ya utalii pia mwenye hapa apate 75% kwasababu yeye ndio mwenye hapa mahali, kuanzia mahotelini, na hata sehemu nyinginezo.Tukija kwa utalii tena utakuta kuna hizi rasilimali zingine kama ndovu. Kweli ndovu ni wazuri wana utalii lakini sisi wanatuudhisana hapa kwetu kwa sababu ndovu anapokula mahindi yako hakuna hata mtu ambaye anakuuliza wala anakuhurumia naanapokuua wewe au akiua mwanao labda wewe utatoa shillingi elfu thelathini. Elfu thelathini ni kitu gani? Sisi tunasema kwambahatuwataki ndovu na kama tunawataka, basi wakiwa wengi wafanywe kama nchi zingine kule Zimbabwe wanachukuliwawanauzwa sehemu zinginezo na nyama zao kuna wengine wanakula nyama za ndovu huko wauziwe hizo nyama za ndovu na sisitupate pesa zirejee hapa kwetu Pwanitupate kunufaika.Lingine ni kwamba katika serikali yetu iliyoko haikujali sana viwanda katika sehemu ya pwani. Utakuta viwanda vingi vimekufahatuna chochote na sasa mwananchi wa kawaida kitu ambacho anakiangalia ni mnazi peke yake. mnazi huu una maneno mengi,mnazi una maarifa yake, mnazi unatilia mboga lakini hakuna mtu ambaye anautambua. Tunasema hata sisi mnazi utambulikekama vile ulivyo kule Malaysia, Mauritius ambako wanafanya vitu vingi kutokana na mnazi.Lingine pia mnazi huu kule ambako wengine tunatoka unatumika kuuzwa na hata watu wakinywa wanalipa skuli ya mtoto. Sasatunasema hii tembo ya mnazi ifanywe kama tembo zingine, ihalalishwe na iwe well done na iuzwe vizuri badala sasa watukufichwafichwa na kushikwa akikutwa anakunywa mnazi. Sasa sisi tunashangaa, mtu amegema tembo lake yuanywa palekando maanake ndio mila yake anashikwa. Mwingine anaenda bar anakunywa busaa mpaka wanakuwa vipofu na hawashikwi.Tunaomba mnazi uhalalishwe ukiuzwa kwa sababu utatufaa hata kupeleka watoto wetu mashuleni.Ninakuja sasa kwa haki za akina mama. Haki za akina mama ninashukuru sana kwamba kina mama tumeambiwa tutoe maoniyetu na sisi tutatoa. Tunataka haki za akina mama ziangaliwe katika sehemu zote. Kuhusu mambo ya uridhi tuangaliwe katika

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!