13.07.2015 Views

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

KERE02-073 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

73kidogo yangu ya kibinafsi. Wakati wa nyuma tulikuwa kuna kitu hapa kwetu kinaitwa ngambi. Ambao ngambi ni kitu ambachotunazuia mimea yetu kama minazi zisiangushwe, ziwekewe muda. Kwa hivyo hicho kitu kinachoitwa ngambi nataka kiwe nisheria na zetu ziangushwe kufuatana na mihula yake ile ambayo watu huangusha zile nazi.Katiba ilinde haki ya mtu asiye na hatia na mtu atakayepatikana na hatia ahukumiwe kulingana na sheria za nchi. Katiba ilindehaki za wananchi kupata elimu ya msingi na bila ya malipo mpaka kiwango cha darasa la nane. Hilo ni oni langu la mwisho.Com. Swazuri: Haya, asante sana Bibi Omar. Na atafuatiwa na bakari.Mr. Bibi Omar: Salaam Aleikum. Mapendekezo ya gender women in development. Kwa jina mimi naitwa Bibi Omar na hii nimapendekezo ya gender women in development. Katika mapendekezo ya akina mama wa gender, utangulizi wa Katiba yetuwa kenya unatakikana uwe hivi. Katiba ni ya wananchi wa kenya walio katika taifa huru lililo jumuisha makabila arobaini namawili yaliyo na haki sawa mamlaka ya juu yawe na wananchi na kenya ni nchi huru yenye mfumo wa vyama vingi natumependekeza mfumo wa Majimbo.Sehemu ya pili- wanawake wawe na mamlaka sawa na wanaume. Rais akiwa mume, makamu awe mwanamke. Mayor akiwamwanamume wa chini wake awe mke na kadhalika. Kwa sababu sisi tunaona wanawake tumezidi na kwa nini tuwetunanyanyaswa na wanaume saa zote? Tumependekeza pia kuwe na idara ya wanawake ambayo itaanzia kutoka wilayanimpaka kwa national na huyu ambaye atakuwa mkuu wa national aweze kuingia Bunge na kutoa maoni ya wanawake wote.Pia tumependekeza wanawake wanaoolewa na mabwana zao kufariki, wakiachiwa mali hiyo ya mabwana zao na watoto,ndugu za hawa mabwana waweze kuwaacha, waishi hapa na watoto wao kwa kuwalea vizuri halafu mali hiyo iwe chini ya huyomama. Tumependekeza pia watoto wanaozaliwa nje ya ndoa washughulikiwe na mababa zao, kielimu, kiafya, mavazi nakadhalika, kuondoa uchokora na wizi mwingi kenya. Wanawake wawekewe wape haki zao ili kuwapunguzia mzigo wa ulevi,umaskini, maradhi ya sasa tuliyonayo.Wakati wa ugawaji wa ardhi, wanawake walioolewa waweze kugawiwa ardhi hizi pamoja na mabwana zao majina yote mawiliyaonekane katika hizo title deeds na mwanamume asiweze kuuza ardhi hiyo bila consultation ya mwanamke. Kesi za dhulumadhidi ya wanawake zihukumiwe na majaji wanawake kwa sababu majaji wanaume wanaonekana saa nyingine wanapendelea.Elimu ya msingi iwe ya bure na pia huduma za hospitali ziwe za bure kwa sababu mzigo huu wote unaenda kwa akina mama,ndio walezi na ndio waangalizi wa nyumba kwa hivyo mizigo mingi huwa inaachiwa wao. Serikali isambaze maji yaani hizihuduma ambazo ni za lazima kwa mwanadamu isambaze maji kwa kila sehemu bure halafu huduma hizi za kudumisha hudumaza maji ziendelezwe na wananchi wenyewe ili wanawake kupunguziwa mzigo wa kutembea sehemu mbali.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!