Views
9 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

kiroho” kusudi lake ni

kiroho” kusudi lake ni “kuwahudumia na kuwanufaisha wengine” ambao Mungu anapenda kuwasaidia kupitia uwezo wake wa kiungu (supernatural means). Jambo muhimu la nne, ni kwamba vipaji vya asili vinahitaji kuendelezwa kwa mafunzo na mazoezi; wakati ambapo “karama za kiroho” zenyewe hutenda kazi kulingana na kiwango cha ukuaji wa kiroho wa mwamini na uhusiano wa karibu wa kiroho kati yake na Mungu. Vipaji Vya Asili Hukaa Katika Nafsi Ya Mtu Katika uchambuzi wa utendaji wa vipaji vya asili na karama za kiroho, tutaona ya kwamba, vipaji vya asili chimbuko lake ni katika nafsi ya binadamu, na chimbuko la “karama za kiroho” chimbuko lake ni katika roho ya binadamu. Hebu tupitie kwa ufupi kuhusu “vipaji vya asili” jinsi vinavyotenda kazi kutokea kwenye nafsi. Ndani ya nafsi ndimo mna vitu vikuu vitatu ambavyo ni akili, hisia na utashi. Kila “kipaji cha asili” kwa asili yake lazima “kitumie akili” ambayo ni sehemu ya nafsi, lazima “kiguse hisia” ambayo sehemu ya nafsi, na lazima kitokane na “utashi wa mtu’ ambao pia ni sehemu ya nafsi. • Ni rahisi kwako kuliko mengine na wengine • Hutumii nguvu nyingi kupita kawaida • Inaeleweka kwa urahisi • Unaona ni kawaida na unashangaa kwanini wengine hawawezi • Unafanya kwa ubora zaidi • Unafanya kwa furaha na shauku ya moyo Karama Za Kiroho Makao Yake Ni Katika Roho Ya Mtu Utendaji wa “karama za kiroho”, tofuati na “vipaji vya asili”, wenyewe chimbuko lake ni katika roho ya binadamu. Kama tulivyojifunza kwamba roho ya binadamu inatokana na vitu 10

vitatu ambavyo ni dhamiri, ushirika na utambuzi. Kwa kuwa asili ya karama za kiroho ni “hali ya kiungu” (supernatural source) na hutenda kazi kutokea ndani ya roho yake. Kwa mujibu wa maandiko matakatifu, tunajifunza ya kuwa Roho Mtakatifu ndiye mdhibiti mkuu wa karama na vipawa vya huduma za kiroho. Hatua ya kwanza kazi ya Roho Mtakatifu ni kumzaa mtu mara ya pili (Yoh. 3:3), na tunafundishwa hali hii ya kuzaliwa mara ya pili hufanyika ndani ya roho ya mtu (Yoh. 3:6). Baada ya Roho Mtakatifu kumzaa upya mtu katika roho yake, hatua ya pili ni kujaa ndani ya mtu na kufanya makao ya kudumu ndani roho ya binadamu. Na humo ndimo utendaji wa karama za Roho pamoja na vipawa vya huduma za kiroho hutokea na kudhihirika katika nafsi ya mtu. 11

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
100 %
100%