Views
5 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Njia Za Kutambua Kipaji

Njia Za Kutambua Kipaji Chako Utangulizi Kujitathmini na kutambua una kipaji gani cha asili si kazi nyepesi. Si tukio la mara moja bali ni mchakato. Na mchakato wenyewe unategemea mambo mengi kuanzia umri wako, mazingira unamoishi na kukulia kimalezi; aina ya watu walio karibu na wewe mfano wazazi au walezi na jamaa wa karibu; kama ni mwanafunzi ni aina gani ya shule, chuo na masomo unayochukua. Yote haya ni mazingira ambayo yana mchango mkubwa kwako katika kufanikisha au kutokufanisha zoezi la kujitathmini na kutambua kipaji chako. Hata hivyo, kwa kuwa kipaji cha asili ni hali ya kuzaliwa nayo, uchunguzi unaonesha kwamba mpaka mtu anapofikia umri wa miaka 14 tayari anaweza kujitathmini na kubaini kipaji chake. Kama mtu hakupatwa majanga ya kuathiri afya yake, uwezo wa vipaji ndani yake huendelea kuwemo ndani kama atadhamiria kujitathmini kwa kutafuta kujua anaweza nini ili kujipanga kupata elimu itakayomsaidia kunoa kipaji chake. Uwezo wa kuzaliwa nao hauwezi kuathiriwa na upungufu wa elimu au uzoefu, japokuwa elimu na uzoefu vinaweza kutumika kuboresha uwezo wa kipaji cha asili alichonacho mtu. Kila mtu amezaliwa na uwezo pekee na maalum ambao humfanya kuwa tofauti na wengine katika jamii. Yafuatayo ni baadhi ya mambo machache ya kukusaidia kutambua una vipaji au kipaji gani: 1. Kitu Gani Kilicho Kushughulisha Sana Utotoni? Kama wewe ni mtu mzima tayari, hasa kuanzia miaka 30 na kuendelea, hebu tumia muda kama dakika mbili kujikumbusha enzi zako za furaha kuanzia shule ya msingi. Ni jambo gani 34

ambapo ushiriki wako ulikuwa unapata furaha sana kiasi kwamba unapokumbuka unasisimka mpaka leo. Na jambo gani hasa lililochukulia muda mwingi na hata kukufanya ukorofishane na wazazi au walimu au watoto wenzako wakati kumbe hilo ndilo ulilokuwa ukilifurahia sana? Pengine ulikuwa unahamasika kushiriki mashindano katika michezo kama mpira wa miguu au riadha. Marafiki zako walikufurahia sana ukiwa katika timu yao wakitarajia watashinda kwa sababu yako. Na wewe uliifurahia sana hali hiyo. Pengine ulikuwa unapendelea sana kuimba kwaya au mashairi au ngoma, na hata kuwa kiongozi wa kwaya au kutunga na kufundisha nyimbo au mashairi. Pengine ulikuwa unapenda sana michezo ya kuigiza na kila mara ulikuwa nyota katika michezo uliyoshiriki. Hapa ni muhimu kutofautisha kupenda kitu kwa sababu kina umaarufu, na kuwa na uwezo wa kufanya kitu hicho kwa viwango vya ubora bila kutumia nguvu nyingi kama wengine. Maana watu wengi wanapenda mambo ambayo wanaona yamewafanya wengine kuwa maarufu na wao wanatafuta umaarufu kwa kuiga lakini hawana uwezo wa kufanya mambo hayo kwa viwango vya ubora. Kumbuka “kupenda sana” ni tofauti na “kuweza sana.” Kwa hiyo, katika kutafakari enzi zako za utotoni, hebu fuatilia ni jambo gani ambalo limeendelea kushika nafsi yako mpaka wakati huu wa ukubwani. Bado unapenda kushiriki mashindano ingawa hivi sasa ushindani wako umeuelekeza labda kwenye biashara mpya, bado unaweza kuwa unapendelea kufanya mambo magumu magumu, na miradi ya kimkakati japokuwa sasa unaifanyia kwenye makampuni ya ushauri. Mpaka hivi sasa, vipaji vya asili hujidhihirisha kupitia mambo tunayopenda sana na tunajikuta tuna uwezo nayo kuliko mengine. 35

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100 %
“Baridi Fusion”: Asili Joto, Myeyungano Nyuklia, Tesla, Free Nishati = Pseudo-Sayansi ? (muhtasari katika Kiswahili) / Cold Fusion, Tesla, Free Energy = Pseudo Science?
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
Valentine_s_Day_Anthology_2015
Please click here to view the postcard. - City of Longwood