Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Kuvibaini Vipawa Vya

Kuvibaini Vipawa Vya Uongozi Ziko nadharia za aina nyingi katika kushughulikia maandalizi ya viongozi. Nadharia moja inadai kwamba uongozi ni kipawa na hivyo hakuhitajiki mafunzo ya kitaaluma ya kuandaa kiongozi. Nadharia ya pili inadai kwamba, uongozi ni taaluma ya kawaida ambayo kila mtu anatakiwa kupitia mafunzo ili apate ujuzi wa kuongoza kwa mujibu wa taaluma yenyewe. Binafsi nimekwisha kuonesha msimamo kwamba, uongozi ni kipawa. Lakini ili kuweza kubaini kipawa cha uongozi lazima uwepo mkakati mahususi wenye kutafuta na kugundua kila mwenye nacho. Kama nilivyokwisha kusema hapo awali, malezi ya kimaadili kwa vijana wa kizazi kipya lazima yaende sambamba na kuvibaini vipawa vya uongozi kwa ajili ya kuvitambua na kutengenezea mazingira ya kutumika kwa wakati muafaka. Mafunzo Ya Kunoa Vipawa Vya Uongozi Baada ya kuvibaini vipawa vya uongozi, hatua inayofuata ni kuandaa mafunzo maalum ya kuvinoa kwa ajili ya matumizi yenye ufanisi unaozingatia viwango vya ubora. Kuvitambua vipawa na kuanza kuvitumia bila mafunzo ni kusababisha vituko katika uongozi. Kipawa kinahitaji kunolewa ili kuweza kuleta matokeo yanayotarajiwa. Ile nadharia kwamba kila mtu anaweza kujifunza taaluma ya uongozi na akaweza kuongoza hata kama hana kipawa, bado ina upungufu. Tunao viongozi wengine waliopata mafunzo ya uongozi na wakapewa uongozi lakina wamekuwa si wabunifu, wala hawana ushawishi kwa wale wanaowaongoza. Lakini mwenye kipawa cha uongozi akipata mafunzo; ni sawa na upanga kunolewa ili kuboresha makali yake wakati wa kutumika. 98

Majaribio Ya Uongozi Baada ya kuvinoa vipawa kimafunzo, ndipo unafika sasa wakati muafaka wa kuvifanyia majaribio ya uongozi. Kuvifanyia vipawa majaribio ya uongozi ni pamoja na kuwapa fursa wenye vipawa kushika nafasi za uongozi kuanzia ngazi za chini na huku wakitathminiwa jinsi wanavyodhihirisha uwezo na sifa zao kabla hawajaanza kuonja madaraka makubwa na ya juu katika ngazi za uongozi. Mbinu mbali mbali za kufanya majaribio ya uongozi ni pamoja na kuunda vyama na jumuiya mbali mbali zitakazotoa fursa za uongozi ili wale wanaojaribiwa wapewe uongozi na kisha wakionekana wameiva waanze kupewa nafasi zile za kiutendaji zisizotakiwa kufanya majaribio. 99

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
Valentine_s_Day_Anthology_2015
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet

“Baridi Fusion”: Asili Joto, Myeyungano Nyuklia, Tesla, Free Nishati = Pseudo-Sayansi ? (muhtasari katika Kiswahili) / Cold Fusion, Tesla, Free Energy = Pseudo Science?
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Nyerere Kuhusu Elimu (Blue BookTF).indd - HakiElimu
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet