Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA MUZIKI 28

Kipaji cha muziki kwa lugha ya Kiingereza ni Musical Thinking ambacho kimebeba uwezo maalum wa kutumia sehemu ya ubongo iitwayo sular ambayo imejaa fikira za muziki na hutumia utambuzi wa ndani wa kufahamu mambo yasiyo dhahiri. Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Muziki Kimauimbile, mtu mwenye kipaji cha muziki, katika mfumo wa ubongo wake anazo seli za neva zenye uwezo wa kuimba au kupiga vyombo vya muziki, uwezo wa kutambua mahadhi na kupambanua mambo yasiyo dhahiri kupitia muziki. Pia mwenye kipaji cha muziki ana uwezo wa kuwasoma watu kwa kusikiliza sauti zao na lugha kupitia maungo ya mwili, na sio kwa kusikiliza maneno peke yake. Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Muziki • Utambuzi wa ndani wa kuhisi wakati mambo ni mazuri au mabaya • Hafanyi mambo mpaka amejisikia yuko sahihi • Hawezi kujieleza lakini ana hisia za kutambua ni nani wa kuaminiwa na ambaye sio • Yuko makini na hisia kali na mazingira na kujisikia au kutojisikia raha katika maeneo fulani • Hutafuta kusikiliza sauti, huvutiwa na muziki, na hupenda kutunga nyimbo/muziki • Uwezo wa kuimba vizuri kwa vina na mjuzi wa kupiga vyombo • Kutunza muda katika kuimba • Uwezo wa kusikiliza na kukosoa muziki • Ukusanyaji wa nyimbo, ala na muziki • Hupenda kuchezesha miguu, vidole au kalamu anapofanya kazi au kusikiliza jambo 29