Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Vitu Muhimu Vya

Vitu Muhimu Vya Kurithisha Elimu Na Ujuzi Zamani za wahenga wetu, urithi ulihusu mali zilizoachwa na marehemu tu. Na hii ndiyo asili ya neno Urithi. Mali au vitu vinavyoachwa na marehemu na kupewa mtu fulani wa ukoo husika. Lakini siku hizi mambo yamekwisha kubadilika. Urithi wa kwanza na wa kudumu ni elimu na ujuzi. Kama tulivyokwisha kusoma sehemu uliyotangulia ya kuwa wajibu wa kurithisha elimu na ujuzi unaanzia katika ngazi ya familia, halafu unakuja kwenye taasisi na kisha ngazi ya kitaifa. Isitoshe, ni haki ya kibinadamu kwa kila mtu kupata elimu ili kujiendeleza kiujuzi. Kwa kuwa kitabu hiki kinahusu vipaji vya asili, huko mbeleni nitaweka bayana ni aina gani ya elimu na ujuzi vinavyotakiwa kurithishwa kama njia ya kuinua na kunoa vipaji. Rasilimali Msamiati wa neno rasilimali umetafsiriwa kuwa ni “jumla ya mali aliyonayo mtu au nchi.” Kama nilivyotangulia kudokeza hapa juu kwamba, rasilimali ndio urithi unaofahamika tangu enzi za wahenga na hata sasa bado umeendelea kuwepo. Hapa inabidi tuzingatie kwamba rasilimali ni mali iliyozalishwa na kumilikiwa na familia. Ni wajibu wa kila familia kufanya kazi kwa bidii, kuchuma mali na kuzimiliki kifamilia. Tufahamu kwamba kiasi cha rasilimali ilichonacho familia ndicho kinachoweza kurithishwa kwa watoto wanapokuwa watu wazima. Ngazi ya pili ya kurithisha rasilimali ni ngazi ya kitaifa. Hapa nikiwa na maana ya serikali ya nchi kuhakikisha kila raia anatengenezewa mazingira ya kumwezesha kuzalisha na kumiliki 90

asilimali kwa njia halali na kwa mujibu wa sheria. Aidha, ni kuhakikisha rasilimali za asili katika nchi zinalindwa kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo; na Kipaumbele katika matumizi ya rasilimali za asili kiwe ni kuwawezesha raia kuwa na haki ya umiliki wake kisheria. Uongozi Tumekwisha kujifunza kwamba uongozi ni mojawapo ya sehemu ya vipaji vya asili. Kimsingi, kipaji hakiwezi kurithishwa toka mtu kwenda mtu mwingine. Muktadha wa “uongozi wa kurithisha” ni ile nafasi au madaraka ya usimamizi na utawala, iwe ni katika taasisi na makampuni binafsi, au katika serikali na taasisi zake za umma. Kwa mantiki hii, uongozi nao ni kitu maalum ambacho kinatakiwa kurithishwa. Japokuwa si kila mtu anaweza kurithishwa uongozi, lakini uongozi kama nadharia na mfumo lazima urithishwe ili kuweza kusimamia masuala ya uchumi na huduma za kijamii kwa raia wa nchi husika. Njia za urithishaji wa uongozi hazianzi na kugawa vyeo vya utawala bila kuzingatia uwezo wa kuongoza. Njia za kurithisha uongozi lazima ziwe na vigezo vilivyo wazi na makini tena kwa mujibu wa sheria na taratibu rasmi, ili warithishwe watu wenye uwezo wa kuongoza. Kama nilivyotangulia kudokeza kabla, ni kwamba nitachambua kwa kina suala la urithithishaji wa uongozi huko mbeleni katika sura hii. Vitu Visivyofaa Kurithishwa Kizazi Kipya Ujinga Kuna usemi uliozoeleka usemao: “Kama unaona elimu ni ghali, basi jaribu ujinga”. Kizazi cha utawala kilichopo hivi 91

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
100%
Finding The Pleasure Free Ebook
GOLDINI