15.11.2012 Views

JUNE, 3RD 2002 - ConstitutionNet

JUNE, 3RD 2002 - ConstitutionNet

JUNE, 3RD 2002 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Wacha we msichana akuwe poleni wacha mama moja akuwe huko mgonjwa kwani tunaona daktari pekee yake na ukweli pia

namna hiyo kwanini lodwar kutoka huko barabara ni lami na hapa kwetu hakuna je magari ngapi nabeba ngombe na gari ngapi

ngapi nabeba ngamia mbusi kwa nini serikali angalie hapa. Hapana mwisho tena kitu moja ngoja wewe ulisema subuhi muonge

dakika tano na mtu ya kuongea na mtu ya kutranslate ndugu yangu ni two minutes na thirty seconds uligawa na dakika hiyo ni ya

mtu moja unaona subuhi nafinya sisi. Ngoja sasa okay sasa,

Ingine ni mambo ya siasa kama Narok hii kweli nafika watu au population ya Mandera iko na minister sisi napewa MP kwa

nini serikali nafinya sisi tunakosa minister moja tafadhali serikali afunguwe macho hatutaki mambo ya dim aone sisi na full lights.

Waziri tunataka na peana (inaudible)---------- mwenyewe Garissa pekee yake hii MP yangu hawezi kumalisia mimi problem

moja aende office ya raisi mbaka ainamie minister ingine what for kwa nini tulichagua tunataka minister yetu nafikiri ile kitu nalete

shida ni kila mwaka tunachagua KANU KANU ndio nalete shida. Basi kwahivyo nyingine police ngoja mimi nilifanya miaka

thelathini na tatu kazi ya serikali hapana kazi ya army na ninaelewa kila corner askari natakikana hata kama namna gani aweke

namba ya police na AP pia iko namba aweke namba yao. Wakifanya maovu askari tu kicomplain hakuna namba nguo ni ya

operation area ngoja kubali tunawajua operation area tukuwe level na wananchi wa Kenya.

Tunastajabika kitu ajabu askari akifanya maovu hana namba tukienda kucomplain ofisi namuambiwa huyu naanza kufanyiwa

parade tafadhli fanya parade namuambiwa huyu alikuwa nakisha pitwa sasa kwa cabin ya magari na muambiwa lala nyuma ya

pasia. Namuambiwa okey huyu alikuwa leave nyumbani na nakisha fanya maovu tunataka askari akuwe na namba. Haya ngoja

mbili tu nabaki ingine ni hii hapa kwetu iko watoto nakisha soma one million najazwa hapa watu ya down country. Mimi mtoto

yangu karibu sita namaliza form four iko C+ iko C- nakosa kazi najaa ofisi.

Hata kama hatutaki mambo ya majimbo serikali nanyima sisi previlage yetu atolee sisi mguu tafadhali awachie sisi chance tukae

na kitako tuvune mvuno ya watoto yetu tuone kwa nini mtoto yangu hapana enda fanya Nyeri office hapa najaa watu ya nyeri

hiyo ni kukanyanga sisi ingine ni mambo ya land tunachagua ma concillor angalia haki ya maskini tunachagua watu iko na njaa

tunaomba mambo ya land maploti arudi kwa committee ya wanainchi hatuwezi kaa sababu macouncillor nanyanyasa sisi mbaya

tunachagua maskini ya kusumbua sisi nauza maardhi na mama naka na watoto kumi pahali kwa hivyo asante sana kama mimi

nakosa watu wasamehe mimi

Com. Swazuri: Haya huyo ni warrant officer. Aya maalim Mohamed hayuko Hussein Isaack hayuko Ahmed Bilo hayuko, Ali

Mohamed hayuko, concillor Hussein ilo hayuko, Councilor Ali Maalim hayuko, Mohamed Ali hayuko, Shek Eunice hayuko,

Bari Elmi hayuko, Concillor Alio Hussein, hayuko, Abdi Rashid Isa ndiyo yule pale huyo hapo ni wawili wewe naitwa nani?

wewe ni Abdi Rashid Isa?.

Abdi Rashid Isa: Kwanza mi naitwa Abdi Rashid Isa nashukuru sana kwa kuwatembelea kwanza sisi hapa Mandera na pia

naunga mkono vile watu wengi hapa wandugu walisema. Naunga mkono vile sasa wenzangu walisema, kwa vile ambaye

waliongea kwa upande wa (inaudible)--------- na upande pia kipande. Ya pili tena ni ile ya land ambaye watu waliongea pia

wenzangu hapo kuna watu ambaye wanakuza maardhi ya wazee ambaye amaka mia moja na mbili ambaye ni clerk council kwa

hivo kitu kama hiyo kwa katika hii katiba sisi hatutaki na ingine tunataka Kadhi yetu ya hapa Mandera apewe vifaa ambaye

inayetosha ambaye anaweza kuhukumu naye na tunataka Kadhi awe na (inaudible)--------- si ati ni Kadhi tu ambaye anajua

Kiarabu peke yake lazima awe amesoma na sheria kwa hivyo ni hayo sina mengi ingine ya kusema ni hayo tu.

82

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!