07.12.2012 Views

12TH JULY 2002 - ConstitutionNet

12TH JULY 2002 - ConstitutionNet

12TH JULY 2002 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

watueleze maoni yao juu ya Katiba mpya ambaye itatusaida kujenga Kenya mpya. Tunajua kwamba Kenya inabahati sana

kwa vile watu wa Kenya wametafuta sana Katiba huu mpya kwa miaka zaidi ya kumi. Na si kawaida kwa nchi nyingi ya Africa

kutengeneza Katiba kama hakuna vita. Lakini hapa kwetu tumebahatika kwa maana Serikali pamoja na watu wote wakenya

walikubali Katiba mpya iandikwe wakati huu ambao tuko na President ambaye yuko mamlakani wakati huu na hakuna mzozo

wowote ilio mbaya zaidi katika nchi hii kwa hivyo tuna shukuru Mungu kwa hayo. Na tunatumaini ya kwamba nyinyi ambao

mulifika hapa mutatusaidia na fakira njema ya kutengeneza Katiba mpya. Sisi kama ma-commissioners hatuko na uwezo

wakuandika Katiba bila kupata ithini na maoni kutoka kwenu. Kwa hivyo tunawashukuru na ku wauliza tafadhali mtuletee

mambo yatakayo tu saidia kuandika Katiba mpya. Asanteni sana.

Com. Ayonga : Asante mama Asiyo, sasa itakuwa Bwana Abubakar Zein.

Com. Abubakar : Habari ya asubuhi. Kama alivyo sema mwenyekiti wa kikao hiki, mimi naitwa Abubakar Zein na mimi

ni mmoja kati ya ma-commissioner wa Tume ya kurekebisha Katiba na kwa ada na desturi zetu za kiafrica wazee wakisha

sema mimi ni kukubali na kuafik na kuyapendekeza waliosema. Asanteni.

Com. Ayonga : Asante Bwana Abubakar Zein. Sasa katika kikao cha leo. Ninataka kumuuliza Bwana Abubakar Zein

achukuwe wadhifa wa mwenyekiti. Yeye ndiye atawaambia taratibu ya kuchukua maoni. Sasa mpaka wakati tutakapomaliza

yeye ndiye atakuwa mwenyekiti. Bwana Zein njoo uketi hapa.

Com. Abubakar : Asante sana Pastor Mzee Ayonga. Kama alivyo sema Mzee amenipa kazi ya kufanya na mimi

nitajaribu kuifanya kwa uwezo yangu. Kwanza kabisa ningependa kuwapa maelezo kuhusu kazi ya leo tutaifanya namnagani,

na kwa haraka kabisa nita waambia kwamba, wale ambao wamekuja hawajajiandikisha waende pale kwa lile dawati pale,

kwenye meza ile ndogo alio kaa ule Binti, wajiandikishe pale. Wale watu wanaojiandikisha pale, wanajiandikisha kwamba

wamefika na kuhudhuria kikao hiki. Na kuna watu aina mbili wanaojiandikisha pale. Wale ambao watatoa maoni leo, na wale

ambao wata kaa kusikiliza tu. We are registering both observers as well as those who have submissions to make. Hilo ni la

kwanza.

La pili, tutakuwa tukitumia ile orodha ya majina tukipata kutoka pale, tutakuwa tukitumia hiyo ili kuwaita watu jinsi walivyo

jiandikisha. Aliyejiandikisha number ya kwanza ataitwa apewe fursa ya kwanza. Halafu nikuaambie ya kwamba sisi kawaida

huwa tunajipa haki kama Tume, ikifika wakati kutakuwa kuna sababu za kutosha kutoka katika orodha hii ya majina. Kando

kidogo kama kwa mfano tupate bibi ambaye ni mjamzito tuta jaribu kumpa fursa ya kuzungumza au mtu Mzee sana, au mtu

ambaye ni mlemavu, au mtu mgonjwa, au mtu yeyote ambaye anasababu ya kutosha kupewa fursa ya kuzungumza mbele, hata

kiongozi wetu yeyote hapa akitokea tutampa fursa azungumze halafu tutarudi kwenye orodha. Au si sawa hivyo? Ikiwa

siwasikii na pengine munaona si sawa. Ni sawa hivyo? Sawa.

5

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!