07.12.2012 Views

12TH JULY 2002 - ConstitutionNet

12TH JULY 2002 - ConstitutionNet

12TH JULY 2002 - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Kiswahili, ambayo ni lugha yetu ya taifa. Lugha ya pili ni kingereza. Lugha ya tatu ni lugha ambayo inazungumzwa hapa. Hapa

inazungumzwa lugha gani? Kipsigis!. Tutatumia kikipsigis kwa mtu ambaye anaona hawezi kuimudu lugha ya kiswahili au ya

kingereza. Anaona atajieleza vizuri zaidi kwa kikipsigis, kutakuwa na mkaleman. There will be somebody to translate from

Kipsigis to Kiswahili or English. Lakini ujue ukitumia mkalemani kwa sababu wewe ukizungumza halafu mkaleman azungumze

time zinaenda hivyo kwa hivyo tuta kuangalia vizuri ukianza kusema maneno mengi sana tutamuaambia mkaleman muambie huyu

Bwana atoe mapendekezo, utasikia. Utanisikia mimi kama mwenyekiti, nafikiri Mzee ameniambia leo niwe mwenyekiti kwa

sababu damu ya ujana inachemka, inasema toa mapendekezo ukianza story nyingi nitakuambia je unapendekeza nini ndugu

yangu. Nausisikie vibaya, au kuna mtu atasikia vibaya hapa? Hakuna.

Lingine la muhimu kufahamu ni kwamba lolote utakalo zungumza hapa unalindwa kisheria. Maanake nini. Maanake kwamba

wewe uko uhuru kusema lolote unalotaka. Hakuna mtu atakaye kufuata baadaye au ofisi fulani ikufuate au Assistant Chief

akufuate, hakuna. Unalindwa kisheria. Sheria inakulinda. Inasema wazi kwamba maoni yako unalindwa. Vile tunavyolindwa

sisi ma-commissioners kufanya kazi zetu, na nyinyi munalindwa kisheria kutoa maoni yenu. Lakini hiyo haina maana kwamba

unauhuru wewe wakuja hapa kumkashifu mtu au kumharibia mtu jina au kumtukana mtu fulani. Maoni yako utazungumzia

mambo muhimu, issues. We are not going to make this a personal forum to attack other people or institutions. Sijui kama

tunaelewana hivyo. Kwa hivyo hatutaki majina ya watu, tunataja mambo tunayotaka ya ingie katika Katiba. Sijui kama

tunaelewana hivyo. Mpaka muniambie kwamba munaelewa ndio mimi niendelee. Sijui tunaelewana hivyo? Ni sawa? Sasa

kufikia hapo kawaida mimi huuliza je! kuna mkenya yeyote aliye hapa ambaye hakufahamu mambo haya au kuna kitu anataka

afafanuliwe zaidi ana swali lolote hapa? Kuna mkenya mwenye swali lolote hapa? Hakuna mkenya yeyote mwenye swali?

Kwa kuwa tunaona hakuna mtu mwenye swali naomba munipe ruhusa nianze kazi na kumuita mtu atakaye tufungulia kikao

chetu leo kama alivyo sema mwenyekiti. Ningependa kukitambua kikao hiki sasa kuwa kikao rasmi cha Tume ya kurekebisha

Katiba ya Kenya kwa minajili ya kukusanya maoni ya wakenya ile kubadilisha Katiba yetu. I would like to officially recognize

this as an official sitting of the Constitution of Kenya Review Commission for the purpose of collection of views of our people to

alter our Constitution. Sasa nikisha sema hivyo kwamba nimekitambua kikao rasmi kinanidhamu yake. Hapa pana kuwa kama

kortini sasa. Watu hawapigi makofi, ikiwa mtu atatoa maoni uyafurahiye, yafurahiye moyoni kwako. Kwa sababu tuna-record

kila kitu. Ukipata nafasi uje useme naunga mkono jambo fulani. Mtu akisema jambo ukasirike, kasirika ndani ya roho yako.

Ikifika zamu yako uje useme jambo lile halikunifurahisha na pinga. Lakini huna haki ya kupiga kelele kumshangilia mtu au

kumzoma mtu. Sasa namuomba Bwana Jeremiah Kirui awe mtu wa kwanza kutufungulia kikao hiki na Bwana Jeremiah Kirui

unadakika tano.

Mr. Jeremiah Kirui Cheruiyot : My name [inaudible]...

Caroline Lang’at : Karibia...

Mr. Jeremiah Kirui Cheruiyot : Hallo, hallo...

7

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!