Read - bunge .parliament.go. tz
Read - bunge .parliament.go. tz
Read - bunge .parliament.go. tz
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
tabia ya kuandika vijinoti kutoka juu kuagiza na kuwaelekeza viongozi wa Serikali za Vijiji kwamba

wawagawie ama wawapimie maeneo hayo na hatimaye kuwamilikisha ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niseme kwamba maadamu nimegongewa hiyo kengele ya

kwanza, niseme haya niliyokuwa nayo yanatosha, niunge mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

MHE. ABBAS Z. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Spika, wakati nikichangia hotuba ya Waziri Mkuu, nilizungumzia maeneo

mawili, Nishati na Madini na Wizara ya Ardhi. Jioni nilipata simu kutoka kwa mama mzazi anaitwa

Bi. Siti Kilungo Mwihiyawe.

SPIKA: Yaani mama yako wewe

MHE. ABBAS Z. MTEMVU: Eeh! Mama mzazi, akaniambia mwanangu mbona umechangia

kwa sauti kubwa sana, mimi sikujielewa, akaniambia angekuwa hai baba yako, asingependa,

angependa uchangie kwa sauti ya taratibu lakini watu waelewe, kwa hiyo sauti yangu leo

itabadilika. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, niwashukuru sana wapigakura wangu wa TMK kwa imani kubwa na

mapenzi makubwa kwangu. Wamekuwa wakipata tabu siku hizi, sasa nisiposema kidogo

wanaweza wasielewe. Wamesikia mambo mengi ya DDC, niwahakikishie huko sipo, mwaka 2009

mwenye dhamana, Mama Celina Kombani aliunda Tume ambayo ina taarifa zote za DDC. Kwa

hiyo, wasiwe na wasiwasi sipo, hizo ni kelele za mlango ambazo hazimzuii mwenye nyumba kulala.

(Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende moja kwa moja Kurasini. Nilichangia wakati wa Waziri Mkuu,

Mheshimiwa Waziri anakumbuka, ndugu zangu wa Kurasini wana matatizo kwelikweli na Waziri

amezungumza kwamba ule mpango wa Kurasini ulianza toka mwaka 2006. Waheshimiwa

Wabunge hebu tuangalie wananchi hawa wanavyopata tabu toka mwaka 2006 leo mwaka 2011

watu hawajalipwa fidia, wanazuiwa nyumba zao kutengeneza hata choo!

Mheshimiwa Spika, nilipata taarifa jana zimenisikitisha kweli, Bwana Afya anapita Kurasini,

wale ambao vyoo vyao vibovu anawatoza faini ya shilingi 40,000 mpaka shilingi 50,000, nimesikitika

kwelikweli. Nilitamani yule Bwana Afya nimfukuze kazi, nikasema taratibu na sheria haziniruhusu,

nisije nikafukuza kazi watu barabarani kumbe taratibu haziniruhusu, nikamuomba Mwenyezi

Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, inasikitisha kweli lakini kilichonisikitisha zaidi ni hotuba ya Mheshimiwa

Waziri katika ukurasa wa 25 naomba ninukuu, inasema:-

“Nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi wa eneo la mradi, ana maana Kurasini, kwa

uvumilivu na ushirikiano wao katika utekelezaji wa miradi …”

Mheshimiwa Spika, mimi nashindwa kuelewa hawa watu wanasubiri pesa zao ili waweze

kuondoka lakini Mheshimiwa Waziri anasema anawashukuru kwa uvumilivu. Mimi kwa sababu

nilichangia hotuba ya Waziri Mkuu, nilitarajia leo Mheshimiwa Waziri angesimama hapa angesema

Bunge likiisha anakwenda kuwalipa hawa watu lakini uvumilivu gani usiokuwa na mwisho Wale

watu wanateseka, hebu tujifikirie tungekuwa sisi, ni bora kama ule mradi hatuuwezi tuwaambie

wananchi wajenge nyumba zao, waendelee kuishi kuliko kuendelea kuwatesa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi napata wasiwasi sana tunapozungumzia mradi wa Kigamboni

na tukionyeshwa picha nzuri. Kama wananchi wa Kurasini, mradi wa kuendeleza bandari toka

mwaka 2006 mpaka leo wananchi wale hawajalipwa, wanapata taabu kwelikweli na cha

kusikitisha zaidi, mimi Temeke nimeshinda kwa kura nyingi 58, lakini Kurasini sikushinda na sababu ni

hiyohiyo ya ule mradi.

60