kwenye Bandari hiyo na kufanya mizigo ya Tanzania tukaichukue kwenye Bandari hiyo. Ina maana tutakosa biashara za Malawi, Zambia, tutakosa biashara zote za transit goods na hivi sasa inaweza ikaonekana mpango wa Kurasini ukafa sababu Serikali itakuwa haina cha kufanya. Sasa naomba Serikali waende wafanye utafiti je, mpango huu upo Maana yake tayari upo, sisi tunajua upo. Nchi hii ya jirani ina-lobby sasa hivi kwa kusema Tanzania meli zinakaa zaidi ya wiki mbili Bandarini. Sio tija kwa meli kukaa kipindi chote hiki, ndiyo maana wanafanya mpango sasa transhipment iwe kwenye nchi yao, watunyang’anye biashara yetu sisi na tukiwa hatuna biashara yetu sisi, sidhani kama kutakuwa na mpango mwingine wa kupanua Bandari, itakuwa hakuna haja kabisa. Kwa hiyo, naomba, Waziri uko hapo na viongozi mpo na watu wanaohusika wapo hebu jaribuni kwenda kutizama tatizo hili. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maneno haya narudia tena kusema sitaunga mkono mpaka tupate majibu, majibu sahihi ya kutazama hali ya watu. Watu wetu wana imani na Serikali, watu wetu wana shida, mkombozi wao ni Serikali. Wanapokuja watu kutokujali watu wa chini, watu wa kuja kudai maslahi yao, wanateseka, mtu anakuwa mpangaji kwenye nyumba baada ya miezi mitano anasoma ndani mle, anakwenda kubadilisha hati ya mazabe, Wizara hii ni wiki moja, hati ya mazabe ni wiki moja, hati halali miaka minane. Bado Makatibu wapo, bado Makamishna wapo, bado watumishi wapo, kila unayemkuta Wizara hii asubuhi anachokonoa meno. Wanakula dhambi na hili hatutalikubali hata siku moja. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka Waziri ameingia ana uzoefu mkubwa sana upo unapotoka, atumie uzoefu wake aachane kabisa na kanyaboya ambao wako kwenye Wizara yake, wasimpotoshe. Pili narudia, hakuna mtu, hakuna kiongozi anayekataa maendeleo ya kwenye Jimbo lake, lakini maendeleo haya lazima ashirikishe viongozi, washirikishwe wadau waliokutwa, wadau waliokutwa waone benefit, waone fruits za mradi huu na wao zinawagusa. Sio unamtoa mtu hapa unamwambia nyie mmevamia ondokeni, watu wako pale miaka 50, hakuna aliyevamia, wote ni wakazi halali wa maeneo yale na nawa-support kama Mbunge wao. Ikibidi kwenda Mahakamani kama hamkutushika, kwanza nchi hii ina viongozi wanne tu; Mwenyekiti wa Mtaa, Diwani, Mbunge na Rais. Waziri sio Kiongozi, Mkuu wa Mkoa sio kiongozi, ni watendaji wanasikiliza maagizo. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka hili mlielewe hatutakubali watu hawa kunyanyasika, kuna watu pale zaidi ya 10,000 hivi saa hizi ninavyozungumza, hawajijui wafanye nini, wamepakata watoto wao tena mama maskini, wamebeba watoto wanalia Yarabi Mungu tusaidie mpango huu usiwepo. Kama mpango huu mnao kweli, wajengeeni makazi, wapeni replacement najua Mheshimiwa Waziri ametoka UN Habitat huruhusiwi kumfukuza mtu mpaka unampa eneo lingine na sio kuwapeleka kwenye hema, mjengeeni pale pale Jangwani. (Makofi) MWENYEKITI: Kengele ya pili Mheshimiwa Azzan. Waheshimiwa Wabunge sasa sijui makofi hayo ni baada ya Mwenyekiti kusimama, kwa maana na yeye yanamhusu. (Kicheko) Waheshimiwa Wabunge naomba nikiri kwamba mmejitahidi kuchangia kwa hisia tofauti, kuwawakilisha wananchi wetu wa Tanzania kwa ujumla wetu kwa maana ya mgawanyo wa Majimbo ya kila mmoja anakotoka na matatizo ya ardhi jinsi yalivyojiri katika eneo lake. Nina imani kabisa Mheshimiwa Waziri amechukua nafasi nzuri ya kusikiliza, basi kesho atakapokuja hapa atakuwa na majibu ya kutosha ili kuweza kutusaidia sisi wawakilishi wa wananchi kwa mujibu wa Katiba, lakini atae maelezo kwa mujibu wa kanuni za Bunge. Muda wetu kwa leo umekwisha, sasa naomba niseme yafuatayo:- Tangazo nililoletewa na Ofisi ya Bunge nimeshawatangazia, lakini naomba tu niseme Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakiwasiliana na wale ambao hawapo. Kwa hiyo, uchangiaji mnaona ile orodha imekwenda katika utaratibu tofauti, lakini ni baada ya kuletewa taarifa rasmi hapa mezani. Kwa hiyo, kesho mchangiaji wetu wa kwanza atakuwa Mheshimiwa Wenje, atafuatiwa na Mchungaji Nshama, atafuata Mheshimiwa Mchungaji Natse, atafuatiwa na Mheshimiwa Susan Kiwanga, nilitaka kusema Mchungaji, lakini Susan bado sio Mchungaji, labda yuko njiani kusomea Uchungaji. 90
Kwa hiyo, baada ya hao niliowataja Makatibu wetu wataendelea kuiweka ile orodha vizuri kama ilivyo na tutaendelea na mjadala huu kesho. Kwa hiyo, baada ya kutoa matangazo haya na maelekezo haya ya Kiti, naomba sasa niahirishe shughuli hizi za Bunge. Waheshimiwa Wabunge, tutakutana tena kesho saa tatu asubuhi, ndani ya Ukumbi huu. Ahsanteni sana. (Saa 12.25 jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumanne, Tarehe 16, Agosti, 2011 Saa Tatu Asubuhi) 91
- Page 1 and 2:
BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADI
- Page 3 and 4:
MHE. REGIA E. MTEMA: Mheshimiwa Spi
- Page 5 and 6:
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANS
- Page 7 and 8:
Mheshimiwa Spika, natumia fursa hii
- Page 9 and 10:
Nyamigege); Maarifa (kijiji cha Ngo
- Page 11 and 12:
Moja ni COPEC ambayo hivi karibuni
- Page 13 and 14:
(c) Mheshimiwa Spika, mwaka 2008 mi
- Page 15 and 16:
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa S
- Page 17 and 18:
Kwa hiyo basi, uamuzi wangu ni kwam
- Page 19 and 20:
Mheshimiwa Spika, napenda kuwashuku
- Page 21 and 22:
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2010/20
- Page 23 and 24:
Vijijini, Kinondoni, Mafia, Mkinga,
- Page 25 and 26:
Natoa wito kwa Halmashauri zote nch
- Page 27 and 28:
Mheshimiwa Spika, kuhusu kuongeza e
- Page 29 and 30:
makazi holela kwa kushirikiana na b
- Page 31 and 32:
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010
- Page 33 and 34:
Mheshimiwa Spika, Wakala wa Utafiti
- Page 35 and 36:
mbalimbali, kwa mfano maonesho, maa
- Page 37 and 38:
Malengo ya Milenia. Hivyo, naomba k
- Page 39 and 40: Mheshimiwa Spika, sita, Idara ya Mi
- Page 41 and 42: Mheshimiwa Spika, nchi nyingi zinaz
- Page 43 and 44: Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa
- Page 45 and 46: utakaogharimu mabilioni za dola la
- Page 47 and 48: kubwa sana. Taarifa za kiuchunguzi
- Page 49 and 50: 1997. Na ili ardhi husika iweze kup
- Page 51 and 52: Sayansi ya Tiba ya Afya (MUHAS) Mlo
- Page 53 and 54: Mheshimiwa Spika, kama ilivyoripoti
- Page 55 and 56: gharama nafuu. Lengo la Wakala ni k
- Page 57 and 58: kuhakikisha kwamba wanaochezea chez
- Page 59 and 60: Mipango Miji, kuendeleza uovu wao m
- Page 61 and 62: Mheshimiwa Spika, tulikwenda na Waz
- Page 63 and 64: na maombi ya kampuni hiyo kuwa kati
- Page 65 and 66: endelevu kutambua maeneo haya na ku
- Page 67 and 68: nafuatilia vizuri Rutoro Muleba kwa
- Page 69 and 70: MHE. MODESTUS D. KILUFI: Basi Mhesh
- Page 71 and 72: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kigamboni, h
- Page 73 and 74: wapo, Majeshi yapo, bunduki zipo la
- Page 75 and 76: wananchi kwamba utaratibu tuliojiwe
- Page 77 and 78: unatokea katika Kata ya Chanika, ka
- Page 79 and 80: hatuwezi kufanya Kwa hiyo, naomba W
- Page 81 and 82: maendeleo Tukijenga Chuo Kikuu kile
- Page 83 and 84: MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, ka
- Page 85 and 86: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepeleka o
- Page 87 and 88: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe
- Page 89: Leo amekuja Mheshimiwa Waziri humu