10.07.2015 Views

Constitution Of Kenya Review Commission [Ckrc ... - ConstitutionNet

Constitution Of Kenya Review Commission [Ckrc ... - ConstitutionNet

Constitution Of Kenya Review Commission [Ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

127tukimbishane na akina baba. Kwa maana sisi wakina mama Waborana kwanza tunafinywa sana sana sana kufinywakwetu ni kutoka asubuhi mwanaume mzima anapanda jukwaa ati mwanamke asisimame kura ya President kwaninihatusimami, hatuna haki? Tunauliza wakina baba, wasiseme hivi tena. Nawaomba ma-commissioners wasiandikehiyo tena, wasiandike kabisa …[ululations]… nawaomba kwa sababu mkiandika kitu kama hii hiyo ni kufunzawasichana wetu kwa shule wasisome. Hiyo ni mbaya, kwanini wamesema hivi hiyo ni mbaya sana, tume kasirikakabisa sisi wakina mama. …[ululations]…Tena kitu kimoja sisi tunataka ni kuhusu wasichana hasa. Wasichana wakichukuliwa kutoka shule sheria ipitishehuyo mtu ametorosha msichana wetu apigwe miaka kidogo kutoka shule sheria mpya aweke hiyo mtu atafanyiwakitu fulani. …[ululations]…Com. Lethome :Pendekeza achukuliwe hatua gani. Pendekeza achukuliwe hatua gani mtu kama huyu?Mama Jamila Bishar : Tutapendekeza hiyo mtu ashtakiwe kwanini ametorosha huyo msichana kamahajamaliza shule hiyo mtu sheria ashtaki mtu kwanza akishtakiwa mtu ya pili hatarudia. Na kama ni mfanyi kaziafutwe kwa kazi yake akae bila kazi kwa sababu ameharibu msichana wetu …[ululations]….Ya pili tena mwanaume akitia msichana wetu mimba sheria mpya ipitishe huyo mtu auwawe …[ululations]… kwasababu hao wavulana ndio wanaleta mfano mbaya kwa wasichana wetu …[ululations]… Auwawe kabisa kwa sababuhiyo ni kuharibu msichana.Tena Katiba mpya ipitishe akina mama wapatiwe nafasi sawa na kina baba kabisa hata kusimama kwa kazi yaPolisi, kwa nini kwa kila kitu. Lakini tunaomba tena katika Katiba mpya wakina mama hawa wa Kiislamuwakiingia kwa kazi mavazi yao hii tu ya Kiislamu sio ya kuamurishwa kuvaa nguo fupi. Kwa sababu ya dini yetu.Dini haiwezi kutukubalia kuvaa nguo fupi tukiwa Polisi tukiwa karani tukiwa mwalimu tukiwa bunge tukiwa ninikwa kila kitu mavazi yetu iwe ni ile ya Kiislamu kabisa Katiba mpya ipitishe hivi.Com. Lethome :Haya mama malizaMama Jamila Bishar : Kwa hivyo tunaomba Katiba mpya aangalie haki ya wakina mama vizuri na watotowasichana wote wasome vizuri na masomo ya bure wapatie wasichana ili wasichana wetu washikane na Wakenyawengine. Hiyo miaka ishirini watu tuliomba hiyo masomo ya bure hasa kwa wasichana wapatiwe free, Katibaipitishe hivi hasa wasichana zaidi zaidi. Asanteni sana.Com. Lethome :Haya Asante mama. Mama Salo Abdi? Salto Abdi haraka haraka tumalize na Kina mama

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!