“Kuhusu vitendo vya ubakaji ambavyo nimevisikia, ni kweli. Tunamshukuru MheshimiwaMbunge kwa kutuletea taarifa hizo na naamini wenzangu katika Wizara husika suala hililitachunguzwa kwa sababu kwa vyovyote vile lazima Jeshi litakuwa na majirani. Kwa hiyo, nadhanitatizo hapa siyo kwamba liko karibu ila ni tabia, kama ni kweli, litashughulikiwa”. Mwisho wakunukuu.Waheshimiwa Wabunge, kwa kuzingatia jibu la Mheshimiwa Waziri, ni dhahiri kwambaMheshimiwa Waziri hakutamka kwamba Wanajeshi wanabaka watoto wa shule, bali alichokisemani kwamba Serikali ilikuwa imesikia na kumshukuru Mheshimiwa aliyeuliza swali kwa kutoa taarifahiyo Serikalini ili iweze kufanyiwa kazi na hatua ziweze kuchukuliwa. (Makofi)Nawaomba Waheshimiwa wote ambao tunajibu maswali au kutoa maelezo humuBungeni kuendelea kuwa na umakini ambao tumekuwa nao kwa ajili ya kufanya shuguli za Bungeletu kuwa bora zaidi.Waheshimiwa Wabunge, huu ndiyo Mwongozo wangu kuhusu suala hili. Nawashukurunikwa kunisikiliza. Tutaendelea kufafanua Miongozo mingine kadri muda utakavyokuwa ukiruhusu.Kwa sababu ya muda, kabla sijamwita Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, naomba sasa nimwite Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bunge,Mheshimiwa Mabumba ili aje kuendeleza hili jahazi hapa mbele. Mheshimiwa Mabumba!Inaelekea kuna mawasiliano kidogo, basi nimwite Msemaji wa Kambi ya Upinzani.MHE. JOSEPH O. MBILINYI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI (WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO): Mheshimiwa Naibu Spika, nina matatizo kidogo ya macho,wakati mwingine unaweza ukaona machozi yanatoka, silii! Ni matatizo kidogo ya macho,nimepata eye infections.Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uhai, afya njema nakunipa fursa ya kipekee ya kufanya maajabu yenye manufaa kwa taifa langu; kwa baraka zake,niliweza kung’ara kwenye sanaa na kuwa nyota wa muziki wa Bongofleva, ukipenda – Hip Hop;kwa uwezo wake leo nimekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na kwa mapenzi yake, mimiMsanii wa Bongofleva sasa nimekuwa Waziri Kivuli wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.(Makofi)NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbilinyi, sekunde tu! Sasa, naomba kumkaribisha MheshimiwaMabumba ili aweze kuendelea.Mwenyekiti (Mheshimiwa Sylivester Massele Mabumba) Alikalia KitiMWENYEKITI: Mheshimiwa, endelea!MHE. JOSEPH O. MBILINYI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI (WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nakushukuru kwa kunipanafasi hii ya kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha maoni na mapendekezo ya KambiRasmi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kwa mwakawa fedha 2011/2012, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99 (7) toleo la 2007.Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua na kuthamini imani na heshima kubwa niliyopewa nawananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Licha ya kuletewa mabomu yamachozi, virungu na bado hakuna yeyote kati yetu aliyeogopa. Uwongo haukuweza kufunikaukweli na hata rushwa haikuweza kurubuni akili. Wananchi kwa umoja wao walijitoa mhangakulinda kura zetu bila woga na hatimaye Dunia nzima inajua na imekubali kuwa mimi ndiye SUGUna CHADEMA si chama legelege, bali ni Chama makini na kinachoaminika mbele ya jamii.(Makofi)Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru na kumpongeza kwa moyo wa dhati kabisa KatibuMkuu wa Chama changu, Dkt. Wilbrod Peter Slaa na Makamanda wote wa CHADEMA nchi nzimakwa kazi kubwa tuliyoifanya katika Uchaguzi Mkuu uliopita na kwa harakati nzito tunazoendelea42
kuzifanya za kuielimisha jamii juu ya haki zao za msingi. Watapiga kelele sana lakini hatutarudinyuma, tunasonga mbele mpaka kieleweke. (Makofi)Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima, namshukuru Kiongozi Mkuu waKambi Rasmi ya Upinzani na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe kwakuniamini na kuniteua kuwa Waziri Kivuli wa Wizara hii nyeti. Namshukuru pia Naibu KiongoziMheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto (Mbunge) na Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani,Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa ushirikiano wao mkubwa wanaonipa katika kutekeleza majukumuyangu ya Kibunge.Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati wadau wote waSekta ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kwa kutuamini na kuthamini kazi kubwa yauwakilishi inayofanywa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hata kuamua kutupa ushirikianomkubwa katika maandalizi ya hotuba hii. Naomba niwatambue baadhi ya wadau hao kwashukrani kama ifuatavyo:- Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Klabu za Waandishi waHabari Tanzania (UTPC), Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Rulu Arts Promotions inayosimamiasanaa na Wasanii wote waliokuja kuunga mkono hotuba hii ya Kambi ya Upinzani. (Makofi)Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya habari, weledi na maadili ya uandishi wa habari. Vyombovya habari ni taasisi muhimu sana katika ujenzi wa Taifa lenye kufuata misingi ya demokrasia nautawala bora. Vyombo vya habari vina dhima kubwa ya kutoa habari na taarifa kwa umma waWatanzania kuhusu mambo yanayohusu maisha yao na vilevile kutoa elimu na burudani. Vyombovya habari ni kiungo muhimu cha kuunganisha jumuiya mbalimbali, kujenga Utaifa, umoja nakuhimiza maendeleo.Mheshimiwa Mwenyekiti, vyombo vya habari kwa ujumla wake, ni taasisi yenye nguvu. Inauwezo mkubwa wa kujenga na vilevile kubomoa ikiwa vitatumiwa na kujiendesha vibaya aukuingiliwa uhuru wake. Hivyo basi, wakati vyombo vya habari vina wajibu wa kufanya kazi kwakuzingatia umakini, weledi na maadili ya uandishi wa habari, Serikali nayo ina wajibu mkubwa wakuhakikisha uhuru na haki za kutafuta na kupata habari vinalindwa.Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiotiliwa shaka kuwa baadhi ya vyombo vya habarivimekuwa vikikiuka kabisa maadili ya uandishi wa habari. Kinachosikitisha zaidi ni pale ambapobaadhi ya Waandishi wa Habari na baadhi ya Vyombo vya Habari na ambavyo vimepewadhamana kubwa na jamii wanapokubali kutumiwa na baadhi ya watu wenye nguvu ama zakisiasa au za kifedha ili kuendeleza ajenda zao binafsi. Hili ni jambo lisilopendeza hata kidogo nahalina mustakabali mzuri kwa amani na maendeleo ya nchi yetu.Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachosikitisha zaidi, vyombo vya habari vya Serikali na hapanalizungumzia Gazeti la Serikali Daily News kuongoza katika ukiukwaji wa maadili ambapo katikakipindi cha mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopita, gazeti hili lilichapisha tahariri ya uchocheziiliyosema, “Kamwe Dkt. Slaa hatakuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”Maoni haya ya Mhariri yalilenga kuleta uchochezi na kujenga hoja kwamba hata kamaWatanzania watamchagua Dkt. Slaa kuwa Rais wao, lakini kamwe hatakabidhiwa jukumu lauongozi, jambo ambalo ni la hatari kwa usalama wa Taifa. (Makofi)Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la hatari zaidi hapa ni kwamba walioendesha vitendo hivivya uchochezi ni Wahariri wa Gazeti la Serikali ambalo lilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwavyombo vingine vya habari nchini.Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi ya upinzani inaitaka Serikali ilieleze Bunge hili Tukufuimemchukulia hatua gani Kaimu Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo ambaye aliidhinisha kuchapishwakwa tahariri hiyo? Je, Idara ya Habari Maelezo iliwahi kuandika barua kwa Mhariri huyu kumuonyakama ambavyo imekuwa ikifanya hivyo kwa magazeti mengine; hata kabla ya habarihaijaandikwa, tayari barua inakuwa imeandaliwa na kinachosubiriwa ni gazeti kuchapishwa nabarua hiyo kufika kwa wahusika? Kama Serikali haijamchukulia hatua, Waziri anaweza vipi kuwana mamlaka ya kuadhibu vyombo vingine vinavyodaiwa kukiuka maadili ya uandishi wa habari43
- Page 7 and 8: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini umeg
- Page 11 and 12: NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiw
- Page 13 and 14: NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA
- Page 15 and 16: Pili, Wakurugenzi na Wakurugenzi wa
- Page 17 and 18: MHE. JOHN J. MNYIKA: Naomba unisiki
- Page 19 and 20: inaongozwa na Mbunge wa Jimbo la Pe
- Page 21 and 22: Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuha
- Page 23 and 24: Mheshimiwa Naibu Spika, Baraza la H
- Page 25 and 26: katika kukuza na kuimarisha Demokra
- Page 27 and 28: wakiwa ni Baraza Kuu la Michezo Bar
- Page 29 and 30: · Kusimamia usambazaji wa machapis
- Page 31 and 32: · Kutoa taarifa katika magazeti ku
- Page 33 and 34: · Kufanya tathmini na ufuatiliaji
- Page 35 and 36: 2011 wakati wa vikao vya Kamati vil
- Page 37 and 38: na Mfuko wa Vyombo vya Habari na Ba
- Page 39 and 40: · Serikali itenge fedha za mafunzo
- Page 41: Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, nape
- Page 45 and 46: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na um
- Page 47 and 48: wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UD
- Page 49 and 50: (iii)(iv)(v)(vi)(vii)Chuo Kikuu cha
- Page 51 and 52: kuendelea kufanya vibaya na kuambul
- Page 53 and 54: Serikali, sasa sisi tayari Umoja wa
- Page 55 and 56: iangaliwe. Tena nashukuru hii Wizar
- Page 57 and 58: kunichagua kuwa Mbunge wao kwa mara
- Page 59 and 60: Mheshimiwa Mwenyekiti, mpira wa mig
- Page 61 and 62: na Academy yake, huyu ndiye mtu wa
- Page 63 and 64: matangazo ya kudhalilisha nchi yetu
- Page 65 and 66: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingin
- Page 67 and 68: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ni
- Page 69 and 70: namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa
- Page 71 and 72: Bunge. Mheshimiwa Waziri Mkuu alipo
- Page 73 and 74: pombe tu, wanaishia kunywa pombe, b
- Page 75 and 76: Nishukuru wafadhili na hasa TBC bas
- Page 77 and 78: ushuru kwenye vifaa vya michezo. Vi
- Page 79 and 80: Mheshimiwa Mwenyekiti, niende TBC,
- Page 81 and 82: Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna
- Page 83 and 84: Je, hawa watu wapo na wanafanya kaz
- Page 85 and 86: hapa Bungeni, yupo kule kwenye ofis
- Page 87 and 88: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natak
- Page 89 and 90: tunakwenda Wizara ya Utamaduni kwa
- Page 91 and 92: MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Wale wen
- Page 93 and 94:
jambo hili la kuhakikisha kwamba ku
- Page 95:
na yakizungumza habari ya interest