wakati yenyewe imeshindwa kuwajibisha Wahariri wa gazeti lake? Uchochezi huu unapaswakukemewa na kila Mtanzania kwa nguvu zetu zote. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kuna tabia imezuka ya viongozi wa Serikali kuvitisha vyombo ya habaripale vinapotoa udhaifu wa Watendaji Serikalini, kama ilivyotokea hapa Bungeni hivi karibuniwakati Mheshimiwa Waziri Ofisi ya Rais (Mahusiano) alipotoa vitisho kwa gazeti la Mwananchi.Kambi ya Upinzani inalaani kitendo hicho na kuitaka Serikali iache mara moja vitisho kwa vyombovya habari. (Makofi)Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo ambalo wote tunatakiwa tulikemee kwa nguvu zetuzote na kila inapowezekana tuwaumbue na tuwataje wale wote wanaoshiriki katika matendohaya ambayo hayana nia njema sio tu kwa tasnia yenyewe ya habari kwa kuipa jina baya nakuipaka matope, bali pia kwa nchi yetu kwani tuna mifano dhahiri hapa Afrika na kwinginekoduniani juu ya athari ambazo zimewahi kutokea vyombo vya habari vilipotumika vibaya. Sotetunakumbuka yaliyofanywa na vyombo vya habari vya Serikali kule Rwanda na maafayaliyotokea.Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Haki ya Kupata Habari. Haki ya kupata habari ni haki yamsingi ya binadamu na inalindwa na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania. Ni haki ambayo inamhusu kila Mtanzania bila ya kujali wadhifa au daraja lake kwenyejamii, umri au jinsia. Mwaka 2006, nataka niamini kwa nia njema kabisa, Serikali ilianzishamchakato wa kutunga Sheria ya Uhuru wa Habari kwa kutoa Rasimu ya Muswada wa Sheria hiyo.Hata hivyo Rasimu ya Muswada huo ilikataliwa na wadau kwa sababu haikukidhi haja walaviwango vya Sheria kama hiyo vinavyotakikana. Mwaka 2007, Serikali iliitikia wito wa Wadau waHabari na Haki za Binadamu wa kutaka kuwepo na sheria mbili tofauti na kutenganisha Rasimuyake ya Muswada wa Sheria ya Uhuru wa Habari na kutengeneza Rasimu mbili, moja ya Sheria yaHaki ya Kupata Habari na nyingine ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari.Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kutenganisha Muswada huo ilikuwa na bado ni muhimusana kwa sababu Sheria ya Haki ya Kupata Habari ni mtambuka na inahusu haki ya Kikatiba yaWatanzania wote. Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ni ya kisekta na inahusiana zaidi nakutoa mwelekeo wa jinsi vyombo vya habari vitakavyofanya kazi nchini.Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato huo ulipata mwitiko mzuri kutoka kwa Wadaumbalimbali wa Habari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu ambao kwa umoja waowalitembea nchi nzima kukusanya mawazo na mapendekezo ya wananchi kuhusu Sheria ya Hakiya Kupata Habari. Walipeleka mapendekezo yao kwa Serikali ili yaweze kujumuishwa katikamchakato wa utungaji wa Sheria.Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa Sheria hii ni muhimusana, kwani itaimarisha utawala wa wazi na uwajibikaji. Utawala ulioshamiri katika mila za usiri ndioulioifikisha Tanzania yetu mahali pabaya. Ndio chanzo cha mikataba mibovu na kushindwa kwauwajibikaji kwa sababu tu Watendaji wabovu wanaweza kujificha katika kinga ya usiri.Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitoa ahadi mwaka hadi mwaka kuhusumchakato wa utungaji wa Sheria hii muhimu lakini hadi leo hatujaona Muswada wa Sheria hiyoukiacha ule ambao wadau wamependekeza. Kambi Rasmi ya Upinzani tunaitaka Serikali kuuletaBungeni Muswada wa Sheria hiyo ndani ya mwaka huu, ili tuujadili na kupitisha Sheria hiyo bila yakukawia zaidi.Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzani tunaitahadharisha Serikali kuwa isijaribukuchakachua hata kidogo maoni hayo ya wadau kwa sababu tumejiridhisha kuwa yana msingina dhamira ya dhati ya kuboresha tasnia nzima ya habari na uhuru wake. Tunachukua fursa hiikuwataarifu mapema wadau wote wa habari kwamba tutakuwa pamoja nao wakati wote waharakati za kushinikiza Muswada huo uletwe Bungeni ndani ya mwaka huu. Tunataka Sheria hiyoipatikane mapema iwezekavyo ikiwa imebeba maoni yote ya wadau.44
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na umuhimu wa kupata Sheria Mpya ya Vyombo vyaHabari, ni muhimu pia kuwapo kwa Sheria inayokidhi mahitaji na inayokubalika kwa jamii yote yawananchi. Sheria ya Habari katu si mali ya Waandishi wa Habari na wamiliki wa vyombo vyahabari pekee yao. Ni Sheria ya Watanzania wote. Hii ni kwa sababu, haki ya kupata na kutoahabari, ni haki ya asili.Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wananchi wanasubiri Sheria mpya ya Habari, Kambi yaUpinzani inaitaka Serikali kuleta Bungeni Muswada wa kufuta Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976kwa kuwa Sheria hiyo ni kinyume na Katiba.Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari. Katika Sera ya Habarina Utangazaji iliyotolewa na Serikali na kupitishwa na Bunge lako Tukufu mwaka 2003, kipengelecha 2.2.2 kinaelekeza kwamba; “Sheria mbovu za habari ambazo zimekuwa zikikosolewa nakulalamikiwa kwa kuwa haziendani na misingi ya kidemokrasia zitadurusiwa, kurekebishwa aukufutwa.” Hivyo basi, Serikali iliahidi kuwa itatunga Sheria mpya zinazoendana na wakati na kukidhimahitaji ya kidemokrasia ya wananchi.Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasisitiza kuwa mapendekezo ya wadau yanakidhi kwakiwango kikubwa ahadi hiyo ya Serikali na wadau walizipitia Sheria 27 zinazogusa habari nakupendekeza Sheria 17 miongoni mwa hizo ama zidurusiwe, zirekebishwe au kufutwa. Kambi Rasmiya Upinzani inaitaka Serikali isiendelee kusuasua katika jambo hili na ilete Muswada Bungeni waSheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ndani ya mwaka huu wa fedha.Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa Shirika linalochapisha Magazeti ya Serikali (Daily Newsna Habari Leo) halina Mtendaji Mkuu, toka alipoondolewa Mtendaji aliyekuwepo. Tangazo lakumtafuta Mtendaji mpya mwenye sifa na hadhi ya kuongoza liliondolewa katika mazingiratatanishi. Hivi sasa Shirika hilo limeyumba kiuongozi jambo ambalo limesababisha kushuka kwauzalishaji. Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kuanzisha mchakato wa kumpata Mtendaji Mkuu waShirika hilo mwenye sifa na hadhi, kabla ya mwaka huu haujamalizika.Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya vijana. Benki ya Taifa ya Vijana ianzishwe.Sehemu kubwa ya watu wa Taifa hili ni vijana, tukiendeleza vijana basi tutakuwa tumeendelezasehemu kubwa ya Taifa. Ni muhimu kama Taifa tuweke vipaumbele vya makusudi vya kibajeti vyakuhakikisha vijana wanapewa kipaumbele cha kutosha na kujengewa mazingira mazuri yakujikomboa.Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuanza kujenga mazingira mazuri ya kuchochea ajira nyingikwa vijana kupitia shughuli za ujasiriamali na shughuli nyingine za kiuchumi, Kambi Rasmi yaUpinzani, inaitaka Serikali ianzishe Benki ya Taifa ya Vijana. Tunapendekeza kuwa mchakato wakuanzishwa kwa benki hiyo uanze ndani ya mwaka wa fedha wa 2011/2012 na benki hiyo iwe namasharti nafuu kwa manufaa ya vijana.Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato wa Baraza la Vijana la Taifa. Kwa mara ya kwanzaSerikali iliahidi kuanzisha Baraza la Taifa la Vijana kupitia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka1996 na tangu wakati huo kila mwaka Serikali imekuwa ikiahidi hivyo hivyo lakini hadi leo hakunakilichofanyika.Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzani haiko tayari tena kuona Serikali hiiikiwapotezea muda vijana wa nchi hii. Tunamtaka Waziri atoe kauli ya moja kwa moja yakuhakikisha kuwa mchakato wa kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Vijana unaanza mara moja naBaraza linapatikana ndani ya mwaka huu wa fedha.Mheshimiwa Mwenyekiti, haja ya mabadiliko Idara ya Maendeleo ya Vijana. Kambi Rasmiya Upinzani inaamini kuwa hali mbaya ya maendeleo ya vijana nchini, pia inachangiwa nauongozi dhaifu usiokuwa na ubunifu wa kutosha wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, ambao kwatakribani miaka 10 umekuwa na watu walewale kwenye nyadhifa takribani zote ikiwemo ile ya45
- Page 7 and 8: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini umeg
- Page 11 and 12: NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiw
- Page 13 and 14: NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA
- Page 15 and 16: Pili, Wakurugenzi na Wakurugenzi wa
- Page 17 and 18: MHE. JOHN J. MNYIKA: Naomba unisiki
- Page 19 and 20: inaongozwa na Mbunge wa Jimbo la Pe
- Page 21 and 22: Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuha
- Page 23 and 24: Mheshimiwa Naibu Spika, Baraza la H
- Page 25 and 26: katika kukuza na kuimarisha Demokra
- Page 27 and 28: wakiwa ni Baraza Kuu la Michezo Bar
- Page 29 and 30: · Kusimamia usambazaji wa machapis
- Page 31 and 32: · Kutoa taarifa katika magazeti ku
- Page 33 and 34: · Kufanya tathmini na ufuatiliaji
- Page 35 and 36: 2011 wakati wa vikao vya Kamati vil
- Page 37 and 38: na Mfuko wa Vyombo vya Habari na Ba
- Page 39 and 40: · Serikali itenge fedha za mafunzo
- Page 41 and 42: Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, nape
- Page 43: kuzifanya za kuielimisha jamii juu
- Page 47 and 48: wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UD
- Page 49 and 50: (iii)(iv)(v)(vi)(vii)Chuo Kikuu cha
- Page 51 and 52: kuendelea kufanya vibaya na kuambul
- Page 53 and 54: Serikali, sasa sisi tayari Umoja wa
- Page 55 and 56: iangaliwe. Tena nashukuru hii Wizar
- Page 57 and 58: kunichagua kuwa Mbunge wao kwa mara
- Page 59 and 60: Mheshimiwa Mwenyekiti, mpira wa mig
- Page 61 and 62: na Academy yake, huyu ndiye mtu wa
- Page 63 and 64: matangazo ya kudhalilisha nchi yetu
- Page 65 and 66: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingin
- Page 67 and 68: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ni
- Page 69 and 70: namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa
- Page 71 and 72: Bunge. Mheshimiwa Waziri Mkuu alipo
- Page 73 and 74: pombe tu, wanaishia kunywa pombe, b
- Page 75 and 76: Nishukuru wafadhili na hasa TBC bas
- Page 77 and 78: ushuru kwenye vifaa vya michezo. Vi
- Page 79 and 80: Mheshimiwa Mwenyekiti, niende TBC,
- Page 81 and 82: Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna
- Page 83 and 84: Je, hawa watu wapo na wanafanya kaz
- Page 85 and 86: hapa Bungeni, yupo kule kwenye ofis
- Page 87 and 88: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natak
- Page 89 and 90: tunakwenda Wizara ya Utamaduni kwa
- Page 91 and 92: MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Wale wen
- Page 93 and 94: jambo hili la kuhakikisha kwamba ku
- Page 95:
na yakizungumza habari ya interest