Download - islamic education panel
Download - islamic education panel
Download - islamic education panel
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
wema na wacha-Mungu, daima atajiona kuwa hajafanya wema

wowote wa kumfanya ahisi kuwa bora kuliko wengine.

Tumehimizwa katika Qur-an (83:26) tushindane katika mema na

tuharakie mambo mema. Wala tusitosheke kwa mema machache

tunayoyafanya.

7. Kujiepusha na Ria

Ria ni ugonjwa mwingine unaoweza kumtoa mtu katika

Uislamu na kumtumbukiza katika ushirikina na unafiki.

Muislamu anatakiwa afanye kila kitendo chema kwa ajili ya Allah

(s.w) kwa matarajio ya kupata malipo kutoka Kwake tu na wala

asifanye wema ili kujionyesha kwa watu. Mtu anayefanya wema

kuwaonyesha watu, hayuko tayari kufanya wema pale ambapo

hapana watu wa kumuona au kumsifu. Muislamu anatakiwa

akumbuke daima kuwa yuko pamoja na Allah (s.w) kila wakati,

naye ndiye mlipaji kwa kila analolifanya na anayajua hata yale ya

siri yaliyoko katika nafsi yake.

Kundi la Harakati halina budi kujiepusha na kujiweka mbali

na ria. Halina budi kufanya mambo yake kwa siri kila

iwezekanavyo. Ikibidi Mwanaharakati au kundi la Harakati lifanye

shughuli zake hadharani, halina budi kujizuia na hisia za kujioa na

kujitukuza kwa kutangaza mazuri yake linaloifanyia jamii.

Katika juhudi za kujiepusha na ria, kila Mwanaharakati

ajitahidi kuficha amali zake njema ambazo hazina lazima ya

kuonekana. Kila mara Mwanaharakati atathmini hisia zake kuwa

anafurahia na kupanda kichwa anaposifiwa na watu wakati

inapobidi afanye wema hadharani, au anafurahia zaidi akifanya

amali zake bila ya kuonekana na watu? Iwapo Mwanaharakati

atagundua kuwa nafsi yake inapendelea kusifiwa na watu, basi

ajirudi haraka na kutubia kwa Mola wake. Hali kadhalika, iwapo

Mwanaharakati atakuwa hafanyi vizuri shughuli zake njema

anapokuwa faraghani kama anavyozifanya akiwa hadharani,

ajirudi haraka na kujihesabu kuwa amefanya ria na atubu haraka

kwa Mola wake.

106