Download - islamic education panel
Download - islamic education panel
Download - islamic education panel
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
(vii) Kusimama na kuonya ni amri ya kuwafahamisha

watu juu ya upweke wa Allah (s.w) kuwa hapana Mola apasaye

kuabudiwa kwa haki ila Allah na kisha kuwafahamisha namna ya

kumuabudu Allah (s.w) pekee katika kila kipengele cha maisha.

Baada ya kufikisha ujumbe huu wa Tawhiid, kwa hekima na

mawaidha mazuri (rejea Qur-an 16:125), Mtume na Waumini kwa

ujumla wanaamrishwa kuwaonya watu juu ya adhabu kali

itakayowafika wale wote watakaoishi kinyume cha Tawhiid –

katika maisha ya akhera.

Pia amri hii ya kuwaonya watu inakwenda sambamba na

kuwabashiria malipo mema watakayopata wasimamishaji wa

Tawhiid katika maisha ya akhera. Kuufundisha Uislamu na kuweka

wazi faida itakayopatikana kwa wale watakaoufuata vilivyo na

hasara itakayowafika wale watakaoukanusha, ni hatua muhimu na

ya msingi mno katika harakati za kusimamisha Uislamu katika

jamii.

(viii) Kutakasa nguo, ni amri inayoashiria kuwa mwenye

kulingania Uislamu anatakiwa awe mfano wa kuigwa kwa tabia njema.

Pamoja na mlinganiaji kutekeleza amri ya kutakasa nguo zake na

mwili wake ili awe kivutio kwa watu atakaokutana nao katika harakati

za kulingania Uislamu, anatakiwa awe na tabia njema itakayovuta

usikivu wa watu. Katika kutekeleza amri hii Mtume (s.a.w) alikuwa

akipendelea vazi jeupe na kujipaka manukato ili asiwe kero kwa watu

kutokana na harufu mbaya inayotokana na nguo chafu na majasho.

Sambamba na usafi huu wa nguo na mwili, Mtume (s.a.w)

alikuwa na tabia njema kabisa.

“Na bila shaka una tabia njema kabisa.” (68:4)

56